JamiiForums

JamiiForums

716.2K subscribers

Verified Channel
JamiiForums
JamiiForums
March 1, 2025 at 10:55 AM
Msemaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Geofrey Tengeneza ameelezea hoja za Mwanachama wa JamiiForums.com kuhusu changamoto za Uandikishaji wa Vitambulisho iliyopo Wilayani Uyui, ambapo amekiri kuna uchache wa Watumishi lakini Serikali inatambua hilo na inalifanyia kazi Amesema “Tumepata Watumishi wapya ambao wameajiriwa kutoka Tume ya Utumishi, wapo kwenye mafunzo Makao Makuu baada ya hapo watasambazwa katika vituo tofauti ili kuongeza nguvu kwenye vituo.” Kuhusu hoja ya kuongeza siku za kujiandikisha kwenye Kata wanazopita amesema wamelipokea na watalijadili katika ngazi ya uongozi, wakati huohuo wameelekeza Vituo vifungwe Saa 11 au 12 Jioni badala ya Saa 9:30 Alasiri kama ilivyopangwa awali Soma https://jamii.app/NIDAUyui
Image from JamiiForums: Msemaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Geofrey Tengeneza...
👍 😢 🙏 3

Comments