
Radio Maria Tanzania
February 25, 2025 at 04:01 AM
LEO FEBRUARI 25 TUNAYAKUMBUKA MAISHA YA MTAKATIFU WALBURGA, MTAWA (779)
Walburga alizaliwa Uingereza, alikuwa dada wa Watakatifu Wilibaldi na Winebaldi (tunayemkumbuka 18 Disemba) ambao wote wawili walifuatana na Mtakatifu Bonifasi (tanuyembuka Juni 5) kwenda Ujerumani kama wamisionari.
Baada ya kujiunga na utawa, Walburga aliombwa kwenda Ujerumani pamoja na baadhi ya masista wenzake na kufungua nyumba ya utawa kule.
Kabla ya kuondoka Sista Walburga alisomea uganga apate kuwasaidia wagonjwa kimwili pia.
Kule Ujerumani akawa Mama Mkuu wa Jumuiya yake ya watawa na wakati ule ule ndugu yake Winebaldi alikuwa Abate wa Watawa wanaume.
Ajabu ni kuwa, baada ya kifo
cha Winebaldi, Askofu wa Jimbo alimwomba Sista Walburga ashike wadhifa wa ndugu yake.
Hivyo Sista Walburga aliyekuwa Mkuu wa nyumba ya Masista akawa pia Mkuu wa Monasteri ya watawa wanaume.
Alifariki mnamo mwaka 779, miaka mitatu tu baada ya kifo cha ndugu yake Mtakatifu Winebaldi (tunayemkumbuka 18 Disemba), akazikwa upande wake katika Kanisa la Parokia mjini Eichstat (Ujerumani).
Habari yake nzuri imeenea sana kwa sababu ya aina ya mafuta yenye nguvu ya pekee ambayo hutiririka kupitia tundu katika mwamba ambao juu yake masalia yake yamewekwa. Husemwa kwamba kwa nguvu ya mafuta hayo.
MTAKATIFU WALBURGA, MTAWA UTUOMBEE.
# RadiomariaTanzania
#mahujajikatikamatumaini
#injilishakwaharaka

🙏
❤️
👍
48