Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

344.5K subscribers

Verified Channel
Radio Maria Tanzania
Radio Maria Tanzania
February 26, 2025 at 06:23 PM
SALA YA KUOMBEA MAKOSA YA KILA SIKU Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina Baba wa Milele, ninakutolea Moyo Mtakatifu wa Yesu, na upendo wake wote na Mateso yake yote na Mastahili yake yote. Kwanza - Kulipia dhambi nilizozitenda leo na wakati wa maisha yangu yote. Atukuzwe Baba... Pili - Kuyatakasa mema niliyoyafanya vibaya leo na wakati wa maisha yangu yote. Atukuzwe Baba... Tatu - kutolea mazuri niliyopaswa kufanya na yale ambayo leo sikufanya na wakati wa maisha yangu yote. Atukuzwe... Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina #radiomariatanzania #injilishakwaharaka #mahujajikatikamatumaini
Image from Radio Maria Tanzania: SALA YA KUOMBEA  MAKOSA YA KILA SIKU  Kwa jina la Baba na la Mwana na ...
🙏 ❤️ 👏 ✝️ 😚 122

Comments