Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

344.5K subscribers

Verified Channel
Radio Maria Tanzania
Radio Maria Tanzania
February 27, 2025 at 04:07 AM
LEO FEBRUARI 27 TUNAKUMBUKA MAISHA YA MTAKATIFU LEANDRI, ASKOFU (600) Leandri alikuwa Askofu wa Sevila (Hispania), mdogo wake, Mtakatifu Isidori (tunayemkumbuka 4 Aprili), alimfuata kama Askofu wa Sevila. Dada yake alikuwa ameolewa na mfalme Leovigildi ambaye alikuwa mfuasi wa uzushi wa Arios, na aliwafukuza Wakatoliki. Hata alimtesa mwanawe Hermenigildi aliyeongoka na kushika dini katoliki. Alimfunga gerezani na alimpeleka Askofu mmoja mfuasi wa Arios kumpa Komunyo. Lakini Hermenigildi alikataa kabisa kupokea Komunyo hiyo kutoka kwa mfuasi wa Arios. Hapo Leovigildi aliamuru Askari wamchinje mwanawe gerezani. Baadaye Leovigildi hakupata raha katika maisha yake, kwa sababu dhamiri ya roho yake hakikuacha kumkaripia ya kwamba amemwua mtoto wake. Alipokuwa karibu kuzimia roho alimwita Leandri, akamwomba amlee mwanawe Rekaredo. Leandri alikubali kwa furaha na punde si punde Askofu Leandri alifanya Mtaguso katika mji wa Toledo (Hispania). Hapo wote waliuapiza uzushi wa Arios. Kazi ingine muhimu sana aliyofanya Mtakatifu Leandri ilikuwa kuibadili Liturujia ya Kihispania. Kwa kufuata mfano wa Makanisa ya Mashariki, aliamua Kanuni ya Nikea isemwe katika Misa ili kupinga uzushi wa Arios. Makanisa mengine ya Magharibi yakafuata baadaye kanuni hiyo ya ibada na mwisho Roma yenyewe ikafuata mfano huo, Mtakatifu Leandri alifariki Sevila Mwaka 600. MTAKATIFU LEANDRI ASKOFU, UTUOMBEE. #radiomariatanzania #mahujajikatikamatumaini #injilishakwaharaka
Image from Radio Maria Tanzania: LEO FEBRUARI 27 TUNAKUMBUKA MAISHA YA MTAKATIFU LEANDRI, ASKOFU (600) ...
🙏 ❤️ 👍 👆 👏 😢 🥰 41

Comments