Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

350.5K subscribers

Verified Channel
Radio Maria Tanzania
Radio Maria Tanzania
February 27, 2025 at 12:10 PM
SALA YA SAA TISA ✝️Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina Yesu, ulikufa, lakini chanzo cha uhai kilitoka kwa ajili ya watu, na bahari ya huruma ilifunguka kwa ajili ya ulimwengu mzima. Ee chemchemi ya Uhai, huruma ya Mungu isiyo na mwisho, ikafunika ulimwengu mzima na ukajimwaga mwenyewe juu yetu. ✝Ee Damu na Maji, yaliyotoka moyoni mwa Yesu kama chemchemi ya Huruma kwetu. Nakutumainia. (Mara tatu) SALA YA KUOMBA HURUMA YA MUNGU Nakimbilia Huruma yako, Ee Mungu mwenye Huruma, uliye pekee mwema. Ingawa dhiki ni kubwa na makosa yangu ni mengi, naitumainia Huruma yako, kwani Wewe ni Mungu wa Huruma na tangu milele haijasikika kamwe, wala Mbingu wala Nchi hazikumbuki kuwa uliicha roho yoyote iliyotumaini Huruma yako. Ee Mungu wa Huruma, ni wewe tu uwezaye kunihesabia haki. Ni wewe usiyeweza kunikataa nitubupo na kuukaribia Moyo wako wenye Huruma ambao haujamkatalia mtu yeyote hata kama ana dhambi nyingi kiasi gani. Kwa kuwa Mwanao alinihakikishia:, " Mbingu na Nchi zingetoweka kwa haraka zaidi kuliko Huruma yangu kukataa kuikumbatia roho iliyo na matumaini" Ee Yesu, Rafiki wa moyo peke ulioachwa, Wewe ni bandari yangu. Wewe ni Amani yangu, Wewe ni Wakovu wangu, Wewe ni mwali mwangavu umulikao njia ya MAISHA yangu. Wewe U kila kitu kwa roho iliyo pweke. Hata roho ikinyamaza, Wewe waijua na kuhifahamu. Unajua udhaifu wetu na unatufariji na kutuponya kama mganga mwema ukituondolea maumivu Ewe uliye stadi wa kazi. Amina Mtakatifu Rita wa Kashia Utuombeee🙏🏻 #radiomariatanzania #injilishakwaharaka #mahujajkatikamatumaini
Image from Radio Maria Tanzania: SALA YA SAA TISA  ✝️Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu....
🙏 ❤️ 👍 ❣️ 😢 😭 🤣 63

Comments