Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

344.5K subscribers

Verified Channel
Radio Maria Tanzania
Radio Maria Tanzania
February 28, 2025 at 03:02 AM
TUSALI SALA YA MALAIKA WA BWANA Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria, Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Salamu Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina. Ndimi mtumishi wa Bwana, Nitendewe ulivyonena. Salamu Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina. Neno wa Mungu akatwaa mwili, Akakaa kwetu. Salamu Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina. Utuombee mzazi Mtakatifu wa Mungu, tujaliwe ahadi za Kristo. Tuombe: Tunakuomba Ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika, kwamba Kristo mwanao amejifanya mtu; kwa mateso na msalaba wake, utufikishe kwenye Utukufu wa ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote na milele. Amina x3 Raha ya Milele, uwape Ee Bwana na Mwanga wa Milele uwaangazie, Wapumzike kwa amani. Amina x3 . #radiomariatanzania #injilishakwaharaka #mahujajikatikamatumaini
Image from Radio Maria Tanzania: TUSALI SALA YA MALAIKA WA BWANA  Malaika wa Bwana alimpasha habari Mar...
🙏 ❤️ 👍 😂 🤣 🤲 74

Comments