Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

344.5K subscribers

Verified Channel
Radio Maria Tanzania
Radio Maria Tanzania
February 28, 2025 at 04:28 AM
LEO FEBRUARI 28 TUNAYAKUMBUKA MAISHA MTAKATIFU ROMAN, ABATE ( 460)NA MTAKATIFU LUPISINI, MTAWA(480) Roman alizaliwa Ufaransa alipokuwa na Umri wa miaka thelathini na mitano, alikwenda kukaa msituni katika mipaka ya Ufaransa na nchi ya Uswisi alichukuwa daftari alimoandika maisha ya Watawa Watakatifu na pia alichukua jembe shoka na mbegu pale msituni alikaa chini ya mti mkubwa akafanya kazi yake kulima kusali na kusoma maisha ya Watakatifu. Nduguye Mtakatifu Lupisini alikuwa na ndoa yake lakini kwanza alifiwa na Mkewe halafu akafiwa na Baba yake akawaza moyoni mwake kufiwa vile na wazee wangu ndiyo ishara Mungu hanitaki nikae zaidi katika dunia, akaondoka akamtafuta ndugu yake mkubwa Romano toka siku hiyo wakawa watu wawili kule, ulikuwa ni kama Utawani punde wengine walitaka kuyafuata maongozi yao wakajenga nyumba za Watawa. Watawa hawa walikuwa wakifuata Sheria za Kasiani walilima mashamba walifunga sana na hata hawakula nyama maisha yao yote, mawazi yao yalikuwa ngozi za Wanyama, ngozi ikawafaa kwa mvua lakini siyo kwa baridi kali, watu kutoka nchi zote za Jirani walikuja kwa Romano na Lupisini kutaka msaada wa sala zao kwa sababu walikuwa wakiwaponya Wagonjwa wengi. Tumehadithiwa kuwa Mtakatifu Romano alifunga Safari Kwenda kusali kwenywe kaburi la Mtakatifu Morisi, Basi jua lilipotua, Mtakatifu Roman alibisha hodi kwa watu maskini na wenye ukoma walimfungulia mlango Mtawa huyu asubuhi walishangaa walipoona wamekwisha pona Ukoma wao, Mtakatifu Romano wakati ule alikuwa amekwisha Kwenda zake lakini walimfuata na wakampata njiani wakamshukuru kwa furaha. Mtakatifu Romano alikufa Mwaka 460 mdogo wake Mtakatifu Lupisini aliendelea kuishi Utawani kwa miaka ishirini, akafa Mwaka 480. WATAKATIFU ROMANO, ABATE NA LUPISINI, MTAWA UTUOMBEE. #radiomariatanzania #injilishakwaharaka #mahujajikatikamatumaini
Image from Radio Maria Tanzania: LEO FEBRUARI 28 TUNAYAKUMBUKA MAISHA MTAKATIFU ROMAN, ABATE ( 460)NA M...
🙏 ❤️ 👍 43

Comments