
Radio Maria Tanzania
March 1, 2025 at 04:29 AM
AHADI ZA JUMAMOSI YA KWANZA YA MWEZI, KWA HESHIMA YA MOYO SAFI WA BIKIRA MARIA
Kila Jumamosi ya Kwanza ya Mwezi, Mama Bikira Maria, kupitia ujumbe wa Fatima ameagiza na kuwaomba Wakristo kuutuliza Moyo wake kwa sala na sadaka.
Ili ujiweke wakfu kwa Bikira Maria na kuwa mali yake safi na chombo kitiifu na kitakatifu cha kupeleka habari njema ya Kristo, unaalikwa kuwa na ibada ya kipekee kila Jumamosi ya Kwanza ya mwezi kwa miezi mitano mfululizo.
Ambapo ili ujipatie rehema Kamili na kujiimarisha kama Askari hodari wa Kristo, unaalikwa kufanya yafuatayo.
1. Kushiriki Sakramenti ya Kitubio (Maungamo)
2. Kusali Rozari Takatifu kwa Tafakari na kwa imani kubwa.
3. Kupokea Ekaristi Takatifu kwa uchaji
4. Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa matumaini makubwa, ukitarajia nguvu ya Mungu iingie ndani mwako, ndipo uwe askari hodari wakutangaza habari njema kwa wengine.
5. Kushiriki Adhimisho la Misa Takatifu.
Ndugu Mkristo mwenzetu, tunakualika kuishi na kuishika Imani yetu kikamilifu, kwa kujiweka wakfu kwa Mama Bikira Maria ili atuongoze kwa Mungu, kwani Mama anapokuvuta kuja kwa Kristo anataka ufikie Utakatifu, unaposali unamkaribia Mungu, Mama Bikira Maria ni njia yetu yakumfahamu Kristo mwanaye na Mungu Baba yetu, hivyo Kupitia yeye anatukutanisha na nguvu ya Mungu.
Mpendwa usidanganyike na yoyote juu ya Imani yako, baki imara, kumbuka Yesu wakati anakata Roho Msalaba, alitukabidhi kwa Mamaye akasema Yohane Tazama Mama na Mama Tazama Mwana.
Mungu na aibariki sala na Ibada yako, kupitia Mama yetu Bikira Maria.
Tumsifu Yesu Kristo .
Radio Maria Tanzania ni shule ya Kanisa.
.
.
#radiomariatanzania
#injilishakwaharaka
#mahujajikatikamatumaini

🙏
❤️
😢
💒
51