
Radio Maria Tanzania
March 1, 2025 at 07:16 AM
SALA YA KILA SIKU KWA MAMA BIKIRA MARIA
Mama wa Mungu Bikira Maria unikubali ninapokuja.
Mimi ni wako ukiwa Mzima.
Mimi ni wako katika msiba.
Mimi ni wako katika mateso.
Mimi ni wako uwapo Msalabani.
Mama wa Mungu Bikira Maria unikubali ninapokuja.
Mama mwenye uwezo unihurumie, uje Mama unisaidie taabuni, uje Mama unisaidie vitani, uje Mama kaa na mimi kila mahali.
Unaweza kunisaidia mwenye huruma Mama wa neema ya Mungu, msaada tunapotafuta wokovu, matumaini yetu duniani, pango la Mbinguni la Watakatifu.
Nani amekuomba asipate msaada wako?
lini umedharau sala za watoto wako? nazidi kulia katika taabu, katika msiba, nikiwa kifungoni, nalia nisaidie ninayo imani na matumaini mlangoni, Mama anipe furaha za mbinguni.
Mama wa Mungu Bikira Maria unikubali ninapokuja.
Mimi ni wako ukiwa Mzima.
Mimi ni wako katika msiba.
Mimi ni wako katika mateso.
Mimi ni wako uwapo Msalabani.
Mama wa Mungu Bikira Maria unikubali ninapokuja.
Salamu Maria x3
#radiomariatanzania
#injilishakwaharaka
#mahujajikatikamatumaini

🙏
❤️
49