CRDB Bank Plc

CRDB Bank Plc

291.9K subscribers

Verified Channel
CRDB Bank Plc
CRDB Bank Plc
February 23, 2025 at 06:50 AM
Pameanza kunoga sasa! Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt.Doto Biteko leo Februari 23, 2024 ameungana na wakimbiaji wa Kili Marathon nchini na wengine kutokea mataifa mbalimbali kama mgeni rasmi akiwa ndani ya jezi ya kupendeza ya CRDB Bank 5KM Fun Run alifika kwenye njia ya kilomita 5 zilizodhaminiwa na Benki ya CRDB na hatimaye kuanzisha rasmi mbio hizo. Dkt. Biteko aliambatana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi ambaye naye alipendeza kwa kuvalia jezi yake ya CRDB Bank 5KM Fun Run. Benki yetu ikiwa sehemu ya tukio hili la kimataifa la Kili Marathoni 2025 imewakilishwa na Mkuu wa Kitengo cha Masoko, Bi Joseline Kamuhanda aliyempokea mgeni rasmi na viongozi wengine kwenye CRDB Bank 5KM Fun Run. #crdb5kmfunrun #crdbbank #tunakusikiliza
🙏 ❤️ 👍 😂 😢 😮 22

Comments