Chama Imara Na Samia
February 19, 2025 at 07:17 PM
*MAMUYA : DK. SAMIA ATASHINDA HATA WAPINZANI WANAJUA*
Mjumbe Kamati Kuu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg. Halima Mamuya, amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan atashinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa amejipambanua kwa kufanya kazi nzuri ya kuleta maendeleo.
Amesema hakuna mgombea atakayesimamishwa na chama chochote cha siasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ambaye hajui kuwa hana uwezo wa kumshinda Dk. Samia katika uchaguzi huo.
Mamuya aliyasema hayo leo February 19, 2025 jijini Arisha alipozungumza na wanawake.
“Ndugu zangu, wazee wangu mmeyasikia mengi ambayo yamesemwa kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Uvhaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhusu kazi anazozifanya Dk. Samia.
“Mimi niwahakikishie kwamba Dk. Samia atashinda na kwa sababu natembea nchi nzima niwaambie hakuna mgombea anayetoka chama chochote chenye akili anayejua kwamba Samia ni mshindani wake kwa sababu hakuna kwa sasa anayeweza kushindana na Dk. Samia Suluhu Hassan,” amesema.
“Dk. Samia amekuwepo katika siasa hii ya utendaji wa kazi katika ngazi ya taifa kuanzia mwaka 2020, yani kama ni Yanga unasema unaifungaje, unashindanaje na Samia,” amesema.
Amesema kuwa siku zote wanawake wakipewa majukumu huyafanya kwa umakini na uaminifu mkubwa.
“Hakuna mama anayeachiwa familia yake nyumbani hata baba akisema hana kitu hatarudi nyumbani akawakuta wana njaa, kwa hiyo siyo tu tunaye rais, bali tunaye mlezi wa nchi.
“Ni mahali gani uliwahi kuona wanawake ni wachochezi wa vita, nchi zote zinazopigana duniani huko, umewahi kumuona mwanamke akichochea vita, sasa huyu ndiye leo tunamkabidhi nchi…amekuja na sera yake ya 4R anataka masikilizano anataka tuelewane, lakini wale anaowaambia njooni chini tukae tuelewane sasa wamegeuka watesi wakubwa…ukitoka jela unasema asante, ukifika mjini unatukana” amesema.
== ==