Wizara ya Afya Tanzania

Wizara ya Afya Tanzania

230.4K subscribers

Verified Channel
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Afya Tanzania
February 24, 2025 at 05:42 PM
RAIS SAMIA AAGIZA UKARABATI WA HOSPITALI YA WILAYA YA KOROGWE Na WAF - Korogwe, Tanga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama kutoa fedha kwa ajili ya kukarabati Hospitali ya Wilaya ya Korogwe (Magunga) ili wananchi wapate huduma bora za afya. Rais Samia ametoa maagizo hayo leo Februari 24, 2025 wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Korogwe katika chuo cha ualimu, ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake mkoani Tanga yenye lengo la kuzindua na kukagua miradi mbalimbali iliyotolewa fedha na Serikali. "Changamoto nyingine iliyotajwa hapa ya ukarabati wa hospitali, na vizuri niko na Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama, juzi tu tulikuwa na mgeni, katika maongezi yetu kuna visenti tumevipata, naomba vimege ulete kwenye hospitali hii Ili vije kufanya ukarabati," ameagiza Mhe. Rais. Rais Samia kesho ikiwa ni siku yake ya tatu ya ziara yake mkoani humo atatembelea na kufungua shule ya wasichana Tanga, kufungua jengo la Halmashauri ya Mji Handeni, kuweka jiwe la msingi mradi wa maji pamoja na kuzungumza na wanamchi.
Image from Wizara ya Afya Tanzania: RAIS SAMIA AAGIZA UKARABATI WA HOSPITALI YA WILAYA YA KOROGWE  Na WAF ...
❤️ 🙏 2

Comments