
Wizara ya Afya Tanzania
February 25, 2025 at 05:46 PM
Wizara ya Afya inaendelea na Kampeni ya Mtu ni Afya awamu ya pili mkoani Arusha ambapo leo Februari 25, 2025 imefanya Mkutano wa hadhara kwa wananchi wa kata ya Sale Wilayani Ngorongoro lengo likiwa kutoa elimu kuhusu masuala ya Afya na mazingira.
Wataalamu wa Afya wametoa elimu kwa Wananchi hao kuhusu masuala ya hedhi salama, usafi wa mazingira, ujenzi na matumizi ya vyoo bora, uzingatiaji wa kunawa mikono na maji tiririka, udhibiti wa utupaji hovyo wa taka, lishe bora, mazoezi ya mwili, nishati safi na matumizi ya maji safi na salama ya kunywa.

❤️
👍
👏
😂
😢
🙏
9