JamiiCheck

JamiiCheck

83.3K subscribers

Verified Channel
JamiiCheck
JamiiCheck
February 18, 2025 at 12:01 PM
Kumekuwapo na Taarifa inayodaiwa kuchapishwa na Mwanahalisi Digital kuwa Tundu Lissu alisema ni mfaidika nambari moja wa maridhiano, hivyo ni muhimu yakawepo. Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu (KeyWord Search) umebaini kuwa Taarifa hiyo imetengenezwa, Si ya Kweli na haijachapishwa na Mwanahalisi Digital. Hata hivyo Chapisho hilo limebainika kuwa na mapungufu kadhaa, ikiwemo ukosefu wa alama ya mistari inayozunguka upande wa juu na mpangilio wa maandishi kwenye kichwa cha habari, tofauti na machapisho rasmi ya chombo hicho. Soma https://jamii.app/LissuMaridhiano
Image from JamiiCheck: Kumekuwapo na Taarifa inayodaiwa kuchapishwa na Mwanahalisi Digital ku...
👍 😢 🙏 🫠 4

Comments