Dimbani Konekti

Dimbani Konekti

206.5K subscribers

Verified Channel
Dimbani Konekti
Dimbani Konekti
February 22, 2025 at 01:38 PM
BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imebadili uwanja na muda wa mchezo namba 167 wa Ligi Kuu NBC kati ya Simba na Azam ambao ulipangwa kufanyika kwenye dimba la KMC Complex Februari 24, 2025 majira ya saa 10 jioni. Sasa ni rasmi mchezo huo utachezwa katika dimba la Benjamin Mkapa saa 1 usiku, huku Bodi ya Ligi wakieleza sababu kuu ya mabadiliko hayo ni kutoa fursa kwa mashabiki na wapenzi wengi wa soka kufika uwanjani kushuhudia mchezo huo unaovuta hisia za watu wengi. Mchezo umetolewa chumbani na kupelekwa sebuleni kila mtu ajionee.😅
Image from Dimbani Konekti: BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imebadili uwanja na muda wa mchezo n...
❤️ 😂 👍 🔥 🙏 👏 😮 ⚡️ 🇹🇿 🔰 88

Comments