Dimbani Konekti

Dimbani Konekti

206.5K subscribers

Verified Channel
Dimbani Konekti
Dimbani Konekti
February 26, 2025 at 11:54 AM
Timu ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ leo itashuka dimbani ugenini dhidi ya Equatorial Guinea majira ya saa 11 jioni, katika mchezo wa kuwania tiketi kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026 zitakazofanyika Morocco. Huu utakuwa mchezo wa pili baada ya ule wa kwanza Stars ikiwa nyumbani Uwanja wa Azam Complex Chamazi, kushinda mabao 3-1 yaliyofungwa kipindi cha pili na Stumai Abdallah na Enekia Lunyamila waliongia wakitokea benchi na lile la tatu la Diana Msewa. Stars ikifuzu fainali hizo, itaungana na timu nyingine za taifa za Tanzania zilizofuzu kwenye mashindano makubwa ya Afrika, Taifa Stars iliyofuzu Afcon, 17 Serengeti Boys iliyofuzu Afcon U17 na Ngorongoro Heroes Afcon U20.
Image from Dimbani Konekti: Timu ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ leo itashuka dimbani ugenini d...
👍 😂 ❤️ 🙏 😢 🇹🇿 👏 😮 33

Comments