
TCRA TANZANIA
February 22, 2025 at 04:09 AM
#sitapeliki
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb.), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampeni ya #sitapeliki iliyozinduliwa Februari 20, 2025, ikilenga kuelimisha Umma kuhusu kujilinda dhidi ya matukio ya ulaghai na utapeli mtandaoni.
Mhe. Silaa ametoa rai kwa wadau wote wa vyombo vya habari kushiriki katika utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu vidokezo vya usalama mtandaoni, ikiwemo kuhakikisha matumizi ya nywila thabiti na tofauti kwa kila akaunti mtandaoni, kutokubofya viunganishi (link) bila kujua vyanzo vyake, kutotekeleza maelekezo ya kutuma pesa au taarifa binafsi bila kuthibitisha unayemtumia.
Pia amesisitiza kuhusu umuhimu wa matumizi ya namba 100 kuwasiliana na Mtoa Huduma, kuripoti majaribio ya utapeli kupitia namba 15040, kuhakiki usajili wa laini za simu kupitia *106#.
#kikaokaziwadauwaserikalitehama2025 #sitapeliki #elimukwaumma #tcratz #nirahisisanakuwasalamamtandaoni
#smarttanzania #tzdigitaltransformation
🙏
❤️
😂
👍
😮
10