
TCRA TANZANIA
February 27, 2025 at 11:19 AM
📌SEMINA YA MATUMIZI SALAMA YA MTANDAO KWA WAZEE
📍PEMBA
🗓️ 26/02/2025
Ofisi ya TCRA Zanzibar ikiongozwa na Bi. Esuvatie - Aisa Masinga imeandaa na kuratibu Semina ya Matumizi Salama ya Mtandao kwa Wazee, ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya "NI RAHISI SANA", inayohamasisha usalama mtandaoni kwa kila mtumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano.
💡 Kupitia semina hii TCRA imewakumbusha Wazee wa Pemba kuhusu vidokezo vya usalama mtandaoni, kama vile matumizi ya nywila thabiti, kutofuata maelekezo ya kutuma pesa au kutoa taarifa binafsi kwa watu wasiowafahamu mitandaoni, kuepuka kubofya viunganishi bila kujua usalama wake, kuhakiki namba zilizosajiliwa kwa vitambulisho vyao vya Taifa kupitia *106#, kuwasiliana na watoa huduma kupitia namba 100 pamoja na kuripoti majaribio ya utapeli kupitia namba 15040.
#tcratz #elimukwaummama #uchumiwakidijiti #klabuzakidijiti #nirahisisanakuwasalamamtandaoni #nirahisisana #sitapeliki #usalamamtandaoni
🙏
👍
😂
6