
TCRA TANZANIA
February 28, 2025 at 04:47 AM
📌MAADHIMISHO YA WIKI YA NUKTA NUNDU - TABORA
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeshiriki kutoa elimu kuhusu usalama mtandaoni kwa wasioona, katika maadhimisho ya Wiki ya Nukta Nundu, yaliyofanyika Mkoani Tabora kuanzia tarehe 18 hadi 21 Februari, 2025.
TCRA inaendelea kutoa elimu ya matumizi salama ya mtandao ili kuhakikisha kila mtumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano anakuwa salama mtandaoni na ananufaika na fursa za maendeleo ya Teknolojia yanayochagiza ukuaji wa Uchumi wa Kidijiti, ambao ukuaji wake unategemea TEHAMA.
#tcratz #elimukwaummama #uchumiwakidijiti #klabuzakidijiti #nirahisisanakuwasalamamtandaoni #nirahisisana #sitapeliki #usalamamtandaoni
😢
😮
🙏
3