Ikulu Zanzibar

Ikulu Zanzibar

50.6K subscribers

Verified Channel
Ikulu Zanzibar
Ikulu Zanzibar
March 1, 2025 at 11:19 AM
RAIS MWINYI:SMZ ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA VODACOM TZ. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Kampuni ya Vodacom Tanzania katika kuharakisha huduma za kidigitali nchini. Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipokutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire na ujumbe wake Ikulu Zanzibar tarehe 1 Machi 2025. Naye , Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania Philip Besiimire ameeleza kuwa Vodacom itapanua huduma zake Zanzibar kwa ajili ya uwekaji wa huduma za kidigitali katika sekta muhimu ikiwemo elimu, afya, na maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Halikadhalika, Besiimire amesema Vodacom Tanzania kupitia Foundation yake itajitolea kuboresha zaidi miundombinu ya kujifunza kielektroniki na kuwawezesha vijana na wanawake kwa ujuzi wa kidijitali na kifedha ikiwemo pia kuunganisha zaidi ya shule 100 Zanzibar ifikapo 2026.

Comments