Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW)
Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW)
February 25, 2025 at 05:00 PM
BODI YA MAGAVANA ISW YAKAGUA MAENDELEO KAMPASI YA KISANGARA Bodi ya Magavana ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Chini ya Uenyekiti wa Bi. Sofia Simba Leo tarehe 25 Februari, 2025 imetembelea na Kukagua Miradi ya maendeleo na Miundombinu ya Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kampasi ya Kisangara, Mwanga, mkoani Kilimanjaro. Mwenyekiti wa bodi Bi. Sofia Simba pamoja na Wajumbe wa Bodi hiyo wameipongeza Menejimenti ya Chuo cha Ustawi wa Jamii kwa kazi kubwa iliyofanyika ya kukamilisha ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi, bwalo la kulia chakula, Uboreshaji wa maktaba ya kusomea, kuongeza ofisi za watumishi na Kuongeza Wahadhiri pamoja na Watumishi waendeshaji katika kampasi ya Kisangara kama ilivyowasilishwa katika ripoti ya Meneja wa kampasi. Bodi ya magavana imevutiwa zaidi na Kukamilika kwa darasa mfano la kujifunzia la Kozi ya Malezi, Makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto inayotolewa katika kampasi ya Kisangara ambacho ni Kituo cha Umahiri wa Kozi hii.
Image from Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW): BODI YA MAGAVANA ISW YAKAGUA MAENDELEO KAMPASI YA KISANGARA   Bodi ya ...
❤️ 🙏 🙌 6

Comments