IAA Tanzania

IAA Tanzania

24.0K subscribers

Verified Channel
IAA Tanzania
IAA Tanzania
February 26, 2025 at 07:07 PM
UNDP, IAA WAJADILI FURSA ZA KIMATAIFA KWA WAHITIMU Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP) kwa kushirikiana na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) limefanya mkutano kujadili fursa za kimataifa kwa wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwaandaa vijana kwa soko la ajira la kimataifa na maendeleo endelevu. Mkutano huo umefanyika leo, katika ukumbi wa Maktaba Chuo cha Uhasibu Arusha na kuhudhuriwa na wataalamu wa UNDP, wahadhiri wa vyuo vikuu, na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali wanaotarajia kuhitimu, huku lengo kuu likiwa ni kuwaelimisha vijana kuhusu namna wanavyoweza kunufaika na fursa za ajira, mafunzo na miradi ya maendeleo inayotolewa na mashirika ya kimataifa kama UNDP. Akizungumza katika mkutano huo, Mwakilishi wa UNDP Tanzania, Shigeki Komatsubara, amesema shirika hilo lina miradi mingi inayowawezesha vijana, ikiwa ni pamoja na mpango wa UNDP Ambassador Fellowship, ambao huwapa wahitimu nafasi ya kufanya kazi na UNDP katika nchi mbalimbali duniani. Amesisitiza kuwa, vijana wana nafasi kubwa ya kuchangia maendeleo kupitia ubunifu, teknolojia, na ujasiriamali, na hivyo ni muhimu kwao kutumia fursa zilizopo ili kuimarisha uwezo wao katika soko la ajira Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamani Sedoyeka, amewataka wanafunzi wasitegemee vyeti na elimu ya darasani pekee kama nyenzo ya kushindana katika soko la ajira la kimataifa, badala yake, amewasisitiza kuwa wabunifu kwa kujifunza ujuzi wa ziada, kutumia teknolojia, na kushiriki katika fursa za kimataifa kama zinazotolewa na UNDP ili kujiimarisha zaidi na kuwa na ushindani wa kimataifa UNDP imetumia mkutano huo kutoa mafunzo kwa washiriki kuhusu namna bora ya kuandaa wasifu (CV), kuandika barua za maombi ya kazi na mbinu za kufaulu usaili wa ajira katika mashirika ya kimataifa Baadhi ya washiriki wa mkutano huo walitoa shukrani kwa uongozi wa chuo kwa kuandaa tukio hilo muhimu. Wanafunzi walikiri kupata maarifa mapya kuhusu fursa za ajira, mafunzo, na ujasiriamali katika mashirika ya kimataifa, na kwamba sasa wana mtazamo mpya kuhusu jinsi ya kujiandaa kwa maisha baada ya kuhitimu masomo

Comments