Tanzania Investment Centre (TIC)
Tanzania Investment Centre (TIC)
February 21, 2025 at 09:19 AM
Uwekezaji Morogoro📍 Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, tumekutana na kufanya mkutano na wawekezaji katika Mkoa wa Morogoro tarehe 20 Februari 2025. Mkutano huu ulihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Kighoma Malima, Mwenyekiti wa Bodi ya TIC, Dkt. Binilith Mahenge, pamoja na wawekezaji na wadau mbalimbali wa sekta ya uwekezaji. Katika Mkutano huu tumejadili njia bora za kukuza na kuimarisha uwekezaji mkoani Morogoro kwa kuzingatia fursa zilizopo. Aidha, mkutano huu ulikuwa ni jukwaa la kubadilishana mawazo kati ya wawekezaji na wadau wengine wa sekta ya uwekezaji kuhusu mikakati bora ya kuendeleza uchumi wa mkoa huu. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima, alisema kuwa mkoa huu ni mojawapo ya maeneo yenye fursa nyingi za uwekezaji kutokana na miundombinu bora na maeneo mengi wazi (Open Spaces) yanayowezesha ukuaji wa biashara na uwekezaji. Akitaja sekta za uwekezaji, Mhe. Malima alisisitiza kuwa sekta ya Utalii, Ujenzi, Kilimo, na Madini zinahitaji uwekezaji mkubwa zaidi ili kuzalisha ajira na kuendeleza uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla. Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa Bodi ya TIC, Dkt. Binilith Mahenge, alieleza kuwa Morogoro imeendelea kuimarika katika sekta ya uwekezaji. Katika mwaka 2024, Morogoro ilishika nafasi ya tano kitaifa kwa ukubwa wa uwekezaji, ikiwa na thamani ya Dola za Kimarekani milioni 447.5.
Image from Tanzania Investment Centre (TIC) : Uwekezaji Morogoro📍   Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kwa kushiri...
🙏 1

Comments