Tanzania Investment Centre (TIC)
Tanzania Investment Centre (TIC)
February 21, 2025 at 05:16 PM
TIC tunashiriki Mkutano wa Kimataifa wa Nchi zinazozalisha Kahawa, unaoendelea katika jijini Dar es Salaam (JINCC) unaifanyika kwa siku mbili tarehe 21 na 22 Februari, 2025. Mkutano huu unawakutanisha viongozi wa nchi mbalimbali, wawekezaji, na wakulima kutoka nchi 25 barani Afrika kwa lengo la kujadili jinsi nchi za Afrika zinavyoweza kushirikiana katika kukuza uzalishaji wa kahawa. TIC tunashiriki katika mkutano na tuna banda katika maonesho kwa lengo la kunadi fursa mbalimbali za uwekezaji kwa ujumla na kilimo cha kahawa. Mkutano huu unatoa fursa ya kubadilishana maarifa na uzoefu kati ya nchi zinazozalisha kahawa, ambapo washiriki wanajadili mbinu bora za kilimo, teknolojia za kisasa, na mikakati ya kuongeza thamani ya zao la kahawa.
Image from Tanzania Investment Centre (TIC) : TIC tunashiriki Mkutano wa Kimataifa wa Nchi zinazozalisha Kahawa, una...
❤️ 🙏 4

Comments