Nuru Ya Imani
Nuru Ya Imani
February 21, 2025 at 12:48 PM
Shalom wapendwa. Karibuni katika masomo yetu ya kila wiki Jumatatu na Ijumaa. Tukizidi kujifunza na kumtukuza Mungu wetu aliye mwema na ambaye fadhili zake zadumu milele🙏. Neno letu la Leo linatoka 🌟 Yeremia 29:11 – “ Kwa maana ninajua mipango ninayo kwa ajili yenu, asema Bwana, mipango ya amani, wala si ya mabaya, ili kutoa tumaini na siku za baadaye.” BHN✨ Ufafanuzi: Ni wazi kuwa wanadamu ili tufikie malengo kadha wa kadha  tunamipango/plan. Wengine huweka mipango ya muda mrefu na wengine huweka mipango ya muda mfupi. Ni ukweli usiofichika wengi mipango haiendi sawa wanaishia kukata Tamaa,kujizira na wengine hutamani hata kujiua 😢! katika andiko hili, Mungu anatuambia kwamba ana mipango mizuri kwa ajili yetu. Hata katika nyakati ngumu, Mungu anajua na ana mipango ya amani na mafanikio kwa maisha yetu. Mipango hii ni ya kujenga, si ya kuharibu. Kumbe Leo Mungu anatukumbusha safari yetu haijafika mwisho, hayo unayoyaona hayaendi ni mipango yako bali upo mpango wa Mungu juu ya maisha yako,ambayo ni mema kabisa. Kumbe tumaini lipo, kumbe unaweza Simama tena, kumbe waweza kusonga tena, sharti ni kumpa Mungu nafasi ndani ya maisha yako. Achilia maisha yako mikononi mwake maana yeye ndio master planner sio wewe ndugu😊. Tunapokuwa na imani kwa Mungu, tunaweza kuwa na hakika kuwa ana mpango mzuri kwa ajili yetu, na kwamba kila hatua tunayochukua inaelekea kwenye ustawi wa kiroho na kimwili. Leo, tafakari hili andiko na jua kwamba Mungu ana mipango ya ajabu kwa maisha yako! 🙌 Tuombe: Ee Mungu wetu uliye Baba wa Mbinguni, asante kwa mipango yako mizuri juu ya maisha yetu.Asante kwa kuwa kwa Neno lako umetufundisha kuwa sio sisi, ila wewe ndie master planner wa maisha yetu. Tunakubali kuwa wewe ni Mungu wa matumaini na amani. Tunakuomba utuonyeshe njia zako na kutufunulia wazi zaidi mipango yako kwetu juu ya (taja eneo ambalo unahitaji Mungu ajifunue /akuonyeshe njia ya kuendea) . Katika jina la Yesu,tunaomba na kuamini imetendeka;  Amina. *Washirikishe wengine – “Mualike rafiki yako leo ili apate kujua mipango ya Mungu juu ya maisha yake.” *Daima Kumbuka: Iwe ni kupitia changamoto au mafanikio, Mungu anakuwa na wewe na ana mpango wa kumtukuza kupitia wewe, hivyo usikate Tamaa wala kuvunjika moyo. Simama na usonge mbele!
❤️ 1

Comments