
Nuru Ya Imani
6 subscribers
About Nuru Ya Imani
πΏ Karibu kwenye Nuru ya Imani π Hii ni channel ya kiroho inayokusaidia kukua katika imani, kuijua Biblia zaidi, na kushuhudia nguvu ya Mungu katika maisha yako! β¨ π Tutakuwa tukishiriki: β Mafundisho mafupi ya Neno la Mungu β Maombi na na ushauri kwa changamoto za kiroho β Ushuhuda wa matendo ya Mungu β Video na sauti za mafundisho π₯ Ushiriki wako ni wa muhimu! Jiunge nasi kwa kusoma, kushiriki, na kualika wengine. Pamoja tunajenga imani yenye nguvu kwa Yesu Kristo! π Mualike rafiki yako leo! Mungu akubariki! πβ¨
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

Shalom wapendwa. Karibuni katika masomo yetu ya kila wiki Jumatatu na Ijumaa. Tukizidi kujifunza na kumtukuza Mungu wetu aliye mwema na ambaye fadhili zake zadumu mileleπ. Neno letu la Leo linatoka π Yeremia 29:11 β β Kwa maana ninajua mipango ninayo kwa ajili yenu, asema Bwana, mipango ya amani, wala si ya mabaya, ili kutoa tumaini na siku za baadaye.β BHNβ¨ Ufafanuzi: Ni wazi kuwa wanadamu ili tufikie malengo kadha wa kadhaΒ tunamipango/plan. Wengine huweka mipango ya muda mrefu na wengine huweka mipango ya muda mfupi. Ni ukweli usiofichika wengi mipango haiendi sawa wanaishia kukata Tamaa,kujizira na wengine hutamani hata kujiua π’! katika andiko hili, Mungu anatuambia kwamba ana mipango mizuri kwa ajili yetu. Hata katika nyakati ngumu, Mungu anajua na ana mipango ya amani na mafanikio kwa maisha yetu. Mipango hii ni ya kujenga, si ya kuharibu. Kumbe Leo Mungu anatukumbusha safari yetu haijafika mwisho, hayo unayoyaona hayaendi ni mipango yako bali upo mpango wa Mungu juu ya maisha yako,ambayo ni mema kabisa. Kumbe tumaini lipo, kumbe unaweza Simama tena, kumbe waweza kusonga tena, sharti ni kumpa Mungu nafasi ndani ya maisha yako. Achilia maisha yako mikononi mwake maana yeye ndio master planner sio wewe nduguπ. Tunapokuwa na imani kwa Mungu, tunaweza kuwa na hakika kuwa ana mpango mzuri kwa ajili yetu, na kwamba kila hatua tunayochukua inaelekea kwenye ustawi wa kiroho na kimwili. Leo, tafakari hili andiko na jua kwamba Mungu ana mipango ya ajabu kwa maisha yako! π Tuombe: Ee Mungu wetu uliye Baba wa Mbinguni, asante kwa mipango yako mizuri juu ya maisha yetu.Asante kwa kuwa kwa Neno lako umetufundisha kuwa sio sisi, ila wewe ndie master planner wa maisha yetu. Tunakubali kuwa wewe ni Mungu wa matumaini na amani. Tunakuomba utuonyeshe njia zako na kutufunulia wazi zaidi mipango yako kwetu juu ya (taja eneo ambalo unahitaji Mungu ajifunue /akuonyeshe njia ya kuendea) . Katika jina la Yesu,tunaomba na kuamini imetendeka;Β Amina. *Washirikishe wengine β βMualike rafiki yako leo ili apate kujua mipango ya Mungu juu ya maisha yake.β *Daima Kumbuka: Iwe ni kupitia changamoto au mafanikio, Mungu anakuwa na wewe na ana mpango wa kumtukuza kupitia wewe, hivyo usikate Tamaa wala kuvunjika moyo. Simama na usonge mbele!

Shalom wana wa Mungu! Tunashukuru Mungu wetu kwa wema wake na fadhili zake nyingi juu ya maisha yetu. Leo hii tunaangalia uwezo wa Mungu katika kufunua yaliyo siri. Ningependa nianze swali hapa "Je, umewahi kupitia wakati ambapo hukuelewa nini kinaendelea maisha yako? Labda ulikuwa na swali lisilo na jibu, au ulichanganyikiwa kuhusu hatua inayofuata?. Je ulichukua hatua gani kupata majibu ya maswali yako? Tunapojaribu kutafuta majibu kwa akili zetu wenyewe, tunagundua kuwa hatuwezi kuona mbele wala kupata mwafaka. Lakini Leo hii tu najifunza kuna mmoja anayejua kila kitu, hata yale yaliyofichwa. Danieli 2:22 inasema: βYeye huufunua yaliyo mazito na ya siri; hujua yaliyomo gizani, na nuru hukaa pamoja naye.β BHN Hii inatufundisha kuwa Mungu ndiye chanzo cha ufunuo na hekima. Hakuna kitu kinachoweza kufichika kwake. Ikiwa kuna jambo linalokutatiza leo, usijaribu kutegemea nguvu zako mwenyewe. Mgeukie Mungu, mwombe akuonyeshe njia, naye atakufunulia." Mungu ana uwezo wa kufunua mambo yaliyofichika na kuyafanya yajulikane. Anajua kila siri kwa sababu hakuna giza mbele yake yeye ni nuru yenyewe. Mwenye uwezo wa kutuonyesha mambo tunayohitaji kujua, kutupa hekima, na kutuongoza katika maamuzi yetu ni Mungu pekee. Tukisoma sura nzima, tunaona jinsi ambavyo Danieli aliomba kwa Mungu na kupokea ufunuo wa ndoto ya Mfalme Nebukadneza,jambo lililowezekana kwa sababu Mungu ndiye mfunuaji wa siri. Hapa tunajifunza kutozitegemea akili zetu bali kumwomba Mungu atupe hekima na ufunuo katika maisha yetu ya kila siku. Tuombe: Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu. Mungu wa nuru na ufunuo, tunakushukuru kwa kuwa hakuna kilichofichika machoni pako. Tunakuomba utufunulie mapenzi yako maishani mwetu, utupe hekima na kuelewa yale tunayopaswa kufanya. Tunaomba nuru yako ing'ae na kuangaza katika kila hali ngumu tunayopitia na utuonyeshe njia sahihi ya kuiendea. Kama ulivyomfunulia Danieli, tunaomba utufunulie mambo mazito na ya siri yanayohusu maisha yetu, huduma zetu, na hatima yetu(ongeza hitaji lako) . Katika jina la Yesu, Amina.

https://www.instagram.com/nuruimani7?igsh=MTluOXE4MjNsc3lmdg==