
Speak Brands
February 12, 2025 at 11:22 AM
Sehem ya pili
riba nafuu Maana kwa nchi zetu izi ni ngumu kukuta serikali imekaa tu na ela(mda wote imeishiwa 😀)
Hii inatuleta kwenye point yetu ya tatu 👉
3.Riba Nafuu
Inawezekanaje sasa kwa Bangladesh kuweza kukopa kwa riba nafuu na Nigeria ikashindwa?
Inawezekanaje kwa China kuweza kusambaza umeme nafuu lakini Kenya inabid ilipe 'double digit interest' ili iweze kufika uko?
Lakini ndani ya Africa hii hii kuna nchi kama Mauritius ambapo interest ya kukopa ni 'single digit' 2% kama China vile!
Wapo wabishi watasema 'Oh Hao Mauritius ni wahindi zaidi kuliko waafrika' wanasahau iki kiwango cha chini cha Riba ata India hakipo!
Morocco pia kiwango cha kukopa kiko chini kama China,tena wabishi watasema 'Oh Hao ni waarabu zaidi kuliko waafrika' wanasahau Misri tu apo viwango viko juu!
Wanasahau Morocco wanaakiba kubwa kwenye mabenki yao kutokana na 'savings' za watu
Je watu wao wamewezaje kusave na Waafrika wengine wameshindwa?
Ni kwamba wanawake wa Morocco walipunguza Uzaaji wao(fertility rate) kutoka watoto 5.5 ya miaka ya 1980s mpaka watoto 3 miaka ya 1990s
Leo hii adi viwanda vya magari(Renault) vimehamishia uzalishaji wake nchini Morocco
Ukweli ni kwamba nchi inakosa uwekezaji pale idadi na ukubwa wa familia ikiwa ni kubwa mno
Sasa tujiangalie kama Taifa,je tumetimiza Aya matakwa matatu ya sisi kuushinda umaskini?
Ayoub Kawambwa
Banker/Advertising Man