
Pinkie Football Universe
February 13, 2025 at 02:57 PM
✍️Kuna siku niliwahi kusema kuwa "kama kuna jambo nilichelewa kuanza kulifuatilia basi ni mpira wa miguu" kwani unanipa raha ambazo sikuwahi kuzipata popote😀
✍️Awali kabisa nawapa pole wale ambao hamkuwepo Goodson's Park kushuhudia 𝙼𝚎𝚛𝚜𝚎𝚢𝚜𝚒𝚍𝚎 𝚍𝚎𝚛𝚋𝚢 (𝙴𝚟𝚎𝚛𝚝𝚘𝚗 𝚟𝚜 𝙻𝚒𝚟𝚎𝚛𝚙𝚘𝚘𝚕), maana ilikuwa ni patashika nguo kuchanika, nyasi ziliwaka moto, palichimbika na maji yalitoka🔥
✍️Mchezo ulitamatika kwa sare ya 2-2, huku kadi za njano zilitolewa za kwenda huku jumla ya kadi nyekundu 3 zilizotolewa, vibe lilikuwa shindili, almanusura watu kuuana, visu nje nje baada ya 𝚄𝚐𝚘𝚖𝚟𝚒 mkubwa kuibuka pale kipyenga cha mwisho kilipopulizwa🤩
✍️Binafsi hii ndio mechi yangu bora ya msimuu huu kwenye 𝙴𝚗𝚐𝚕𝚒𝚜𝚑 𝙿𝚛𝚎𝚖𝚒𝚎𝚛 𝙻𝚎𝚊𝚐𝚞𝚎 au wewe unasemaje🥳🥳
#𝐏𝐢𝐧𝐤𝐢𝐞4𝐋𝐢𝐟𝐞