
Ashraf JK 💚💙
February 28, 2025 at 05:16 AM
Utafiti mpya umebaini mfumo wa asili wa mwili unaosaidia kupunguza uvimbe wa mishipa ya damu na hatari ya atherosclerosis, ugonjwa unaosababisha magonjwa ya moyo na kiharusi. Watafiti wamegundua kuna protini fulani ina uwezo wa kuzuia mkusanyiko wa mafuta kwenye mishipa ya damu na kupunguza uvimbe unaohusiana na atherosclerosis. Protini hio inajulikana kama IGFBP6.
Atherosclerosis hutokea wakati mafuta na seli zinazoharibika zinapokusanyika kwenye kuta za mishipa ya damu, jambo linaloleta msukumo mkubwa wa damu na kuongeza hatari ya mshtuko wa moyo. Watafiti wanasema kuwa kuelewa protini hii ya asili kunaweza kusaidia kutengeneza tiba mpya za kuzuia ugonjwa huu hatari.
Matokeo haya yanaweza kubadili mbinu za matibabu kwa kutoa njia mpya za kuimarisha ulinzi wa mwili badala ya kutegemea tu dawa kama statins. Wanasayansi wanapendekeza utafiti zaidi ili kubaini jinsi protini hii inaweza kutumika kama tiba ya kibioteknolojia.
Kwa kuwa magonjwa ya moyo yanasababisha vifo vingi duniani, utafiti huu unatoa matumaini ya kuboresha mbinu za kinga na tiba, kupunguza vifo, na kuongeza muda wa kuishi kwa watu walio katika hatari kubwa ya atherosclerosis na matatizo ya mishipa ya damu.
#kmt
#ashrafjk
#afyatamu