
Friends of Dr. Doto Biteko(KNK)
February 8, 2025 at 03:27 PM
*RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI UKUMBI SHULE BUKOMBE*
📌*Awapongeza wananchi kwa kuwa na ukumbi wa kisasa*
📌 *Ampongeza Rais Samia kwa jitihada zake za kuboresha elimu nchini*
*Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati*
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewapongeza wananchi wa Wilaya ya Bukombe hususan Kata ya Bulangwa kwa kuwa na ukumbi wa mzuri na wa kisasa utakaotumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii.
Rais Kikwete amesema hayo leo Februari 8, 2025 katika Kata ya Bulangwa, Wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita wakati akiweka jiwe la msingi katika jengo la ukumbi lililopo katika Shule ya Sekondari Bulangwa.
Akieleza kuhusu ukumbi huo, Rais Kikwete amesema kuwa Dkt. Biteko alifurahishwa na ukumbi wa Shule ya Sekondari Lugoba uliopo katika Wilaya ya Chalinze, Mkoa wa Pwani ambao ulijengwa na Kampuni na MMsteel hivyo alizungumza na Kampuni hiyo na baadae ujenzi wa ukumbi wa Bulangwa ulianza.
“ Niwapongeze sana wananchi wa
