
Friends of Dr. Doto Biteko(KNK)
338 subscribers
About Friends of Dr. Doto Biteko(KNK)
Chaneli rasmi ya marafiki wa Mh Dr.Doto Mashaka Biteko Official WhatsApp channel of Dr. Doto Mashaka Bitekoโs Friends KUSEMA NA KUTENDA (KNK)
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Oman ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 44 ni wa kihistoria na umeendelea kuwa na manufaa baina ya nchi hizo mbili. Dkt. Biteko ameyasema hayo leo Februari 28, 2025 ofisini kwake Jijini Dar es salaam wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Oman nchini, Mhe. Saud Hilal Al Shidhani. " Mhe. Balozi tunakushukuru kwa namna tunavyoshirikiana na uwepo wako nchini umeendelea kuimarisha mahusiano na Serikali yako. Tunafurahia kuwa na uhusiano huu wa kidiplomasia. Sisi tunaichukulia Oman kama marafiki na Mhe. Rais Samia anapenda ushirikiano baina ya Tanzania na nchi zingine, kanuni inayosema ukitaka kwenda mbali nenda na wenzako ni muhimu sana, amesema Dkt. Biteko. Amendelea kusema kuwa uwepo wa idadi kubwa ya Watanzania wanaofanya kazi chini Oman ni tafsiri ya urafiki na ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo.


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa pamoja na dunia sasa kuweka mkazo ikiwemo ya kifedha kwenye uzalishaji umeme kwa kutumia nishati jadidifu kama vile jua, maji na upepo, nchi za Afrika zinapaswa kutumia vyanzo ilivyonavyo kama vile makaa ya mawe ili kuweza kuwa na umeme wa kutosha. Dkt. Biteko amesema hayo leo Februari 11, 2025, New Delhi, India wakati akishiriki katika mjadala wa Mawaziri wa Sekta ya Nishati kutoka India, Qatar, Uingereza na Tanzania wenye mada iliyosema Mpango Mpya wa Dunia wa Biashara ya Nishati ikiwa ni sehemu ya Mkutano wa Wiki ya Nishati India. Dkt.Biteko ametolea mfano kuwa Tanzania ina madini ya makaa ya mawe ya kutosha pamoja na urani ambayo yanafaa kuzalisha umeme hata hivyo kumekuwa na changamoto ya kupata ufadhili wa kuyaendeleza kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa vile yanatajwa kusababisha uchafuzi wa mazingira akieleza kuwa makaa ya mawe yanaweza kutumika kuzalisha umeme kwa kutumia teknolojia ya kisasa yenye kuondoa sumu ya kabon
