Friends of Dr. Doto Biteko(KNK)
Friends of Dr. Doto Biteko(KNK)
February 8, 2025 at 03:44 PM
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ameupongeza uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) Wilaya ya Bukombe kwa Mkutano Mkuu Maalum wa kutoa taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM Jimbo la Bukombe kwa mwaka 2020-2025. Rais Mstaafu Kikwete ametoa pongezi hizo leo Februari 8, 2025 wakati akihutubia katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika katika kata ya Igulwa, Wilaya ya Bukombe, mkoani wa Geita. “Nawapongeza kwa kuandaa mkutano huu, kwa kuwa unakidhi takwa la katiba ya CCM kwa kuwa inawezesha kupima mlipotoka, mlipo na mnapokwenda, katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la 2022 katika Ibara ya 72 (1) inatambua kuwa Mkutano Mkuu ni kikao kikubwa cha Chama katika ngazi ya wilaya, aidha Ibara ya 74 imetamka kazi za msingi za Mkutano huu kuwa ni kuzungumza mambo yote yanayohusu ulinzi na usalama na maendeleo kwa ujumla katika wilaya.” Amesema Rais Kikwete. Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya CCM Bukombe amempongeza Rais Mhe. Dkt. @SuluhuSamia kwa kutoa fedha nyingi zilizosaidia utekelezaji wa idadi kubwa ya miradi ya maendeleo katika Jimbo hilo. Amebainisha kuwa miradi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa inaonekana na ina faida kwa wananchi huku akieleza jitihada za Dkt. Biteko za kuleta maendeleo katika Jimbo hilo. “ Naomba kuwahakikishia kuwa hamkufanya makosa kumpa kura zenu Dkt. Biteko, naomba niwaambie kuwa mambo haya mazuri ya Bukombe yasingetokea kama msingemchagua Dkt. Biteko.” Aidha, Rais Kikwete amewaasa wananchi wa Bukombe kuwachagua wagombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ili kuendeleza miradi ya maendeleo katika Jimbo hilo. Katika hatua nyingine, Rais Mstaafu Kikwete amemshukuru na kumpongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake mzuri wa nchi na kuwa nchi imetulia na ina amani na maendeleo yanaonekana katika kila eneo.
🙏 1

Comments