
Friends of Dr. Doto Biteko(KNK)
February 10, 2025 at 04:52 AM
Aipongeza Al- Hikma kwa kukuza Mashindano ya kuhifadhi Qur’aan Tukufu
* Mashindano ya Qur’aan Tukufu kufanyika mwezi ujao
* Mashindano ya Qur’aan Afrika yawa Mashindano Makubwa Zaidi ya Qur’aan Tukufu Ulimwenguni
Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewaasa waislamu nchini kuendelea kumcha Mungu na kutenga muda wa kujifunza na kuisoma Qur’aan Tukufu ambayo itawafunza mambo mema yaliyoelekezwa na Mwenyezi Mungu.
Dkt. Biteko amesema hayo leo Februari 9, 2025 jijini Dar es salaam wakati akizindua Mashindano Makubwa zaidi ya Qur’aan Tukufu Ulimwenguni 2025.
“ Nawaomba msivunjike moyo akitokea mwenye tafsiri tofauti nyie msivunjike moyo wala kukatishwa tamaa bali mfanye mashindano haya yawe kinara na kuutangaza uislamu katika ulimwengu,” amesema Dkt. Biteko.
Pia amewahimiza kumuomba Mungu ili Qur’aan iwanyanyue na isiwabwage katika shughuli mbalimbali wanazofanya kama kaulimbiu ya mwaka huu inavyosema “ Qur’aan Ikunyanyue, Isikubwa
