Friends of Dr. Doto Biteko(KNK)
Friends of Dr. Doto Biteko(KNK)
February 11, 2025 at 05:03 PM
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa pamoja na dunia sasa kuweka mkazo ikiwemo ya kifedha kwenye uzalishaji umeme kwa kutumia nishati jadidifu kama vile jua, maji na upepo, nchi za Afrika zinapaswa kutumia vyanzo ilivyonavyo kama vile makaa ya mawe ili kuweza kuwa na umeme wa kutosha. Dkt. Biteko amesema hayo leo Februari 11, 2025, New Delhi, India wakati akishiriki katika mjadala wa Mawaziri wa Sekta ya Nishati kutoka India, Qatar, Uingereza na Tanzania wenye mada iliyosema Mpango Mpya wa Dunia wa Biashara ya Nishati ikiwa ni sehemu ya Mkutano wa Wiki ya Nishati India. Dkt.Biteko ametolea mfano kuwa Tanzania ina madini ya makaa ya mawe ya kutosha pamoja na urani ambayo yanafaa kuzalisha umeme hata hivyo kumekuwa na changamoto ya kupata ufadhili wa kuyaendeleza kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa vile yanatajwa kusababisha uchafuzi wa mazingira akieleza kuwa makaa ya mawe yanaweza kutumika kuzalisha umeme kwa kutumia teknolojia ya kisasa yenye kuondoa sumu ya kabon
Image from Friends of Dr. Doto Biteko(KNK): Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema ...
🙏 1

Comments