Friends of Dr. Doto Biteko(KNK)
Friends of Dr. Doto Biteko(KNK)
February 15, 2025 at 07:50 PM
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini India na kuzungumza na Watumishi katika ofisi hiyo. Akizungumza katika Ofisi hizo jijini New Delhi, Dkt. Biteko amempongeza Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega kwa mapokezi mazuri na kazi nzuri zinazofanywa na Ubalozi huo ikiwemo kutangaza fursa za uwekezaji. " Nakushukuru kwa mapokezi mazuri mliyotupatia tangu tulipofika hapa kwa kweli yamerahisisha utekelezaji wa majukumu yetu, mnaipa heshima kubwa Serikali kwa namna ambavyo Ofisi hii inavyohudumia watu mbalimbali wenye uhitaji wanapokuja hapa ikiwemo watu wanaoonesha nia ya kuwekeza Tanzania au Watanzania wanaotaka kuwekeza hapa India." Amesema Dkt. Biteko Amesema ushiriki wa Wizara ya Nishati katika Mkutano wa Wiki ya Nishati India umekuwa na manufaa mbalimbali ikiwemo kuhamasisha ushiriki wa wawekezaji mbalimbali katika duru ya tano ya kunadi vitalu vya mafuta na gesi asilia.
Image from Friends of Dr. Doto Biteko(KNK): Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametembe...

Comments