Friends of Dr. Doto Biteko(KNK)
February 16, 2025 at 02:53 PM
DKT. BITEKO AWAHIMIZA WATANZANIA KULIOMBEA TAIFA
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuiombea nchi pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
“ Tuendelee kuliombea kanisa, tuendelee kuiombea nchi yetu na Rais wetu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambae kwa kweli anafanya kazi nzuri na sisi tunaofanya kazi karibu naye tunaona,” amesema Dkt. Biteko.
Dkt. Biteko amesema hayo leo Februari 16, 2025 wakati akishiriki ibada katika Kanisa la Africa Inland Church Chang’ombe jijini Dar es salaam.
Amewahimiza Watanzania kudumisha upendo na amani nyakati zote hususan kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, ili uchaguzi huo usiwe sababu ya kuligawa Taifa kutokana na tofauti ya mitazamo.
Amesisitiza “ Mungu ametupa bahati ya kuwa na nchi yenye amani, sisi tuilinde kwa wivu mkubwa kwa kuwa amani ikiondoka gharama yake ni kubwa. Tuziombee pia n