Friends of Dr. Doto Biteko(KNK)
February 19, 2025 at 06:38 PM
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko ameagiza Mwanafunzi Mirabelle Msukari na wenzake wa Shule ya Msingi Sun Rise iliyopo Kinondoni mkoani Dar es Salaam wapelekwe katika ziara ya mafunzo kwenye Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), ili wajifunze zaidi kwa vitendo namna mradi huo unavyozalisha umeme.
Dkt. Biteko ametoa agizo hilo kwa njia ya simu baada ya Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga kutembelea shule, hiyo kwa lengo la kumpongeza mwanafunzi huyo ambaye video yake ilijizolea umaarufu kupitia mitandao ya kijamii baada ya kuelezea kwa ufanisi juu ya miradi mbalimbali ya umeme inayotekelezwa nchini ukiwemo wa Julius Nyerere.
‘’Sisi tukupongeze na tumefurahi kwa umri wako unafuatilia masuala ya nishati, sasa tutakupeleka kuliona Bwawa la Julius Nyerere, uone umeme unavyozalishwa ili uendelee kujifunza zaidi. Sisi tunatamani kukuona ukifanikiwa zaidi,” amesema Dkt. Biteko
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (TAN
🙏
1