
Friends of Dr. Doto Biteko(KNK)
February 28, 2025 at 03:25 PM
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Oman ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 44 ni wa kihistoria na umeendelea kuwa na manufaa baina ya nchi hizo mbili.
Dkt. Biteko ameyasema hayo leo Februari 28, 2025 ofisini kwake Jijini Dar es salaam wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Oman nchini, Mhe.
Saud Hilal Al Shidhani.
" Mhe. Balozi tunakushukuru kwa namna tunavyoshirikiana na uwepo wako nchini umeendelea
kuimarisha mahusiano na Serikali yako. Tunafurahia kuwa na uhusiano huu wa kidiplomasia. Sisi tunaichukulia Oman kama marafiki na Mhe. Rais Samia anapenda ushirikiano baina ya Tanzania na nchi zingine, kanuni inayosema ukitaka kwenda mbali nenda na wenzako ni muhimu sana, amesema Dkt. Biteko.
Amendelea kusema kuwa uwepo wa idadi kubwa ya
Watanzania wanaofanya kazi chini Oman ni tafsiri ya urafiki na ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo.

🙏
1