NURU YA UPENDO
NURU YA UPENDO
February 10, 2025 at 03:32 PM
*MAOMBI YA USIKU.(JUMATATU.10.02.2025)* Shalom.Shalom. *NENO KUU* :1 Timotheo 2:1-2 "Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;-kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu." Maombi Ya kila Siku Usiku Kuanzia saa Moja sio Ya kufunga unakula Chakula chako.ukitaka kulala./KUPUMZIKA unaomba vipengele hivi. ✓ Mshukuru Mungu Kwa Siku Nzima Ya Leo Jumatatu Kwa Matendo Makuu Aliyoyenda. 1 Wathesalonike 5:18. ✓Omba Toba na Rehema . ✓Omba Utakaso Wa Roho ,Nafsi na Mwili . *VIPENGELE VYA MAOMBI LEO JUMATATU.TUNAOMBEA FAMILIA NA TAIFA LETU.* *1•Maombi* ya Familia kwa upande wa Nuru iangaze.( *Yohana 1:1-5).* ✓vyote vilifanyika Kwa Yeye(YESU),mwambie Mungu kupitia Mwanaye Yesu afanye maisha Yako kuwa mapya ,Kiroho, familia, kiuchumi,kielimu, kiafya, kitabia, kimwenendo n.k ✓Ndani yake Kuna uzima(YESU),Mwambie Mungu kwa Jina la Yesu Alete uzima kwa Kili kilichokufa kwenye familia Yenu ,mfano elimu, kazi ,uchumi, Watoto, Alete uzima . ✓Muombe Mungu afufue Vyote vilivyokufa katika familia, Mahusiano kati ya ndugu, Wazazi , marafiki, ata ndoa. ✓Uzima Huo ulikuwa Nuru, Muombe Mungu Nuru iliyo na uzima ipite kila Kona ya maisha ya familia wafanikiwe kiroho, kiuchumi, kielimu, kiafya n.k √ Nayo Nuru ikaang'aa Gizani Wala Giza halikuweza ,Muombe Mungu ili Nuru yaani kristo Yesu apite kwenye Kona ya maisha palipo na Giza nuru Yake ikaang'aaze katika biashara, elimu , uchumi, ndoa, Wazazi, Watoto n.k ✓vunja na kuharibu magonjwa ,vifo, Mauti , madhahabu yanayoleta vicheko.geuza vililio kwao, ubaya wote ugeuze kuwa wema, laana ,maagano n.k *3.Kuombea Taifa* ✓Omba Mungu Mwaka huu Alete Amani , umoja, ushirikiano ulinzi, usalama, katika Nchi ukawepo kwa Hali ya juu. ✓Vunja na kuharibu mafuriko ya mvua kwa baadhi ya mikoa, Majanga, vifo ,ajali, Mauti, malango ya Kuzimu na Giza, vita visivyo rasmi, na magonjwa ya milipuko. ✓Omba Mungu Kwa Wamama Wajawazito Kupitia matumbo Yao Tamka Baraka wakazae Watoto Watakao Mjua Sana Mungu Na Kusaidia Taifa Letu. ✓ Vunja roho za Operesheni Kwa Wamama Wakati Wa Kujifungua •Vunja roho za Vifo Kwa Wamama Wakati wanapojifungua . •Vunja roho za Vifo Kwa Watoto wakati wamama Wanapojifungua . *N.b* . Funika nyumba Yako ,Kazi Yako, Elimu Yako ,uongozi wako ,ndugu zako, Watoto wako ,Kwa Damu ya Yesu .Na Vunja Kila maagano na uchawi na laaana Kwa Jina la Yesu . Mungu akitupa Neema kesho vipengele vitatumwa .USIKU MWEMA. Mungu akubariki.
🙏 ❤️ 👍 👏 9

Comments