
NURU YA UPENDO
21.2K subscribers
About NURU YA UPENDO
Karibu katika channel yetu, ya mafundisho ya Neno la Mungu ya Kila siku. Kwa msaada wa kiroho/ kuchangia kazi ya MUNGU, wasiliana nasi kwa namba hizi +255693036618/ +255789001312
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

Ni tunda lipi la Roho unalolipenda zaidi?(Wagalatia 5:22)

https://wingulamashahidi.org/2021/11/15/furaha-ni-nini/ *Furaha ni nini?* Furaha kwa tafsiri ya kawaida, ni muhemko chanya wa kihisia unaotakana na aidha kuridhishwa na jambo fulani au kupata kitu fulani. Kwa mfano katika biblia Wale mamajusi walipoina tena ile nyota ya Bwana kule Bethelehemu, walifurahi. Mathayo 2:10 “Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno”. Utaona pia wale waliokwenda kaburini kwa Yesu,Na kukuta ameshafufuka, Biblia inasema walifurahi sana. Mathayo 28:8 “Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa hofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake habari”. Hata mbinguni malaika wanapoona mtu mmoja ametubu dhambi, huwa wanafurahi pia. Luka 15:10 “Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye”. Kwahiyo utaona hapo furaha tunayoijua, huwa inazaliwa kutokana na kupatikana kwa kitu fulani kilichokuwa kinatarajiwa au jambo fulani. Lakini furaha halisi ya ki-Mungu. Ni furaha inayozidi mipaka, , hata katika shida furaha hii ipo. Ni furaha ambayo huwezi kuielezea kwa upatikanaji tu, kama furaha nyingine, inazidi mipaka hiyo.. Kwa kifupi ni kuwa haiathiriwi na hali au mazingira. Na furaha yenyewe inaletwa na KRISTO YESU mwenyewe. Ikiwa na maana mtu anayempokea Kristo, kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. Mungu anakuwa na jukumu la kumininia furaha hii kwa Roho Mtakatifu atakayempokea kipindi hicho. Warumi 15:13 “Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu”. 1Nyakati 16:27 “Heshima na adhama ziko mbele zake; Nguvu na furaha zipo mahali pake”. Wagalatia 5:22 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria”. Luka 2:10 “Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; 11 maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana”. Yokobo 1:2 “Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; 3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi” 1Petro 4:13 “Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe”. Kwa muda wako pitia vifungu hivi 1Petro 1:8, Yohana 17:13 Na wewe ikiwa ni mmojawapo wa wale wanaotaka kuonja FURAHA hii ya Ki-Mungu ambayo si watu wote wanaweza kuonjeshwa utakuwa umefanya uamuzi wa busara sana. Kwasababu ni kwake tu peke yake ndipo Furaha inapopatikana, hakuna mwingine, Bwana anasema hivi; Zaburi 5: 11 “Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga daima kelele za furaha. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia”. Zaburi 51:12 “Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi. Unaona? Basi fungua leo moyo wako, Kristo aingie ndani yako, kukusamehe, na kukuwekea furaha idumuyo. Ikiwa Upo tayari leo kutubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba. Bwana akubariki. Wafilipi 4:4 Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini. Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312


Jaribio la upendo kama sehemu ya tunda la Roho. Je! Unawaombea wanaokuudhi?

🔥Matokeo Inaonekana wengi wetu tumechagua *UPENDO* . Vema sana, ki-uhalisia yote ni muhimu, lakini pia Upendo humeza mambo mengi. 👇🏾 1 Petro 4:8 _[8]Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.__

🌿 **Asili na upendo wa ki-Mungu* 📖 * 1Wakoritho 13:4-7* Upendo wa ki-Mungu; 1. **Hauna ubinafsi** – Unawatanguliza wengine. (Wafilipi 2:3-4) 2. **Huvumilia** – Upo tayari kungojea hata nyakati ngumu (1 Wakorintho 13:4) 3. **Unafadhili** – unakuwa tayari kusaidia wengine haja zao ( Waefeso 4:32) 4. **Unasemehe** – Hauhifadhi kumbukumbu ya mabaya ya mtu, wala hauoni uchungu (1 Wakorintho 13:5) 5. **Haufurahii mambo mabaya** – Unafurahi kwa yale yaliyo ya kweli tu, (1 Wakorintho 13:6) 6. **Hustahimili** – Vishindo na maudhi haviutikisi (1 Wakorintho 13:7) 7. **Una uaminifu** – hauna ukomo wa kupenda, au unafiki. (Hosea 2:19-20) 8. **Una utakatifu** – Unachipuka katika msingi wa utakatifu (1 Peter 1:15-16) 9. *Haubagui* - Unawapenda na kuwaombea mpaka maadui (Mathayo 5:43-48) 💡 *Upendo wa ki-Mungu hausukumwi na hisia, bali ni unachagua kupenda kama Kristo alivyopenda bila sharti lolote, yaani unajitoa sadaka, kwa wengine. www.nuruyaupendo.com

https://wingulamashahidi.org/2023/11/17/usikwepe-chuo-cha-utakatifu/ *USIKWEPE CHUO CHA UTAKATIFU.* Zawadi kubwa Mungu aliyompa mwaminio ni UTAKATIFU. Utakatifu ni ile hali ya kuwa mkamilifu kama Mungu, kutokuwa na dosari au kasoro yoyote, msafi asilimia mia moja, bila kosa lolote ndani yako. Sasa heshima hii tumetunukiwa na Mungu, jambo ambalo hapo zamani halikwepo, ilihitaji matendo ya haki ya Mtu kuufikia, lakini hapakuwahi kutokea mwanadamu yoyote aliyeweza kufikia cheo hicho cha juu sana cha Mungu, yaani kutokuwa na dhambi kabisa. Lakini pale tunapomwamini Bwana Yesu, siku hiyo hiyo, Mungu anatufanya Watakatifu kama yeye, haijalishi bado tutakuwa na asili ya dhambi nyingi kiasi gani. Hiyo ndio maana ya neema. Tunaitwa watakatifu bila ya kujisumbua kwa lolote. Lakini sasa lengo la Mungu sio tuwe “watakatifu katika dhambi” Bali “tuwe watakatifu katika utakatifu”. Hivyo kuanzia huo wakati anaanza kumfundisha mtu kuusomea hadi kuuhitimu Utakatifu wake, aliopewa ili aendane na cheo alichotunukiwa tangu mwanzo. Na hapo mtu akishindwa kupiga hatua, basi anaondolewa heshima hiyo kwake, na hivyo hawezi tena kuwa kama Mungu, na matokeo yake wokovu unampotea. Mwaka Fulani hapa nchini kwetu kulikuwa na askari mmoja aliyeonyesha kitendo cha kishujaa kukataa rushwa ya milioni 10, ambapo alishawishiwa aipokee ili aifute kesi ya watuhumiwa wawili waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka,. Lakini yeye hakukubali, na ilipokuja kubainika, mkuu wa jeshi la polisi (IGP) akafurahishwa naye, Akampandisha cheo (kwani alikuwa ni askari wa chini). Lakini cha kushangaza baada ya kama miaka miwili tukaja kusikia Yule askari aliyepandishwa cheo ameshushwa cheo kile. Kufuatilia ni kwanini imekuwa hivyo? Jeshi la polisi likatoa taarifa kuwa alionyesha utovu wa nidhani, wa kukataa kwenda kwenye mafunzo ya cheo chake kipya. Akidhani kwasababu IGP amempandisha basi inatosha hakuna haja ya mafunzo tena. Akasahau kuwa ufahamu wake wa kielimu ni lazima uendane na cheo chake, kwamba akiwa bado na cheo kikubwa, wakati huo huo anapaswa aendelee kusoma,na kujifunza kimatendo, ili aweze kutumika ipasavyo. Lakini akashushwa cheo na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kukataa kutii amri ya jeshi. Ndivyo ilivyo katika UTAKATIFU tunaopewa na Mungu bure, ni lazima tuutendee kazi kwa kila siku kupiga hatua mpya ya mabadiliko. Huwezi kusema umeokoka (wewe ni mtakatifu), halafu maisha yako ya mwaka jana na mwaka huu ni yaleyale wewe sio mtakatifu. Kila siku lazima uwe na mabadiliko, ulikuwa unabeti, unaacha kubeti, ulikuwa unavaa mavazi ya uchi uchi, unayachoma moto, ulikuwa unajichubua, unaacha, ulikuwa unasengenya unakaa mbali na wasengenyaji, ulikuwa unakesha kwenye muvi usiku kucha unaacha hayo, unatumia muda wako mwingi kwenye kujisomea biblia, ulikuwa ni mtu wa rushwa unaanza kuondoa vitendo hivyo kwenye biashara yako. Ulikuwa huwezi kufunga na kuomba unaanza kujizoeza kuwa mtu wa rohoni, unafunga, unaomba, na kukesha, Huko ndiko Mungu anakokutaka. Anaona umekiheshimu cheo alichokupa. Ukiwa ni mtu wa kupiga hatua kila siku, basi Mungu atazidi kukuona wewe ni MTAKATIFU na hivyo utakuwa karibu na yeye. Lakini ukiishi hoe hae, hutambuliki kama umeokoka, au vipi, tabia zilezile za zamani unaendelea nazo, wala hujihangaishi kuziondoa. Usijidanganye wewe umeokoka. Bwana atusaidie.. Je! Upo ndani ya Kristo? Je unataarifa kuwa hizi ni siku za mwisho? Yesu amekaribia kurudi? Ni nini utamweleza Mungu siku ile endapo leo utaukataa wokovu unaoletwa kwako bure.. Tubu dhambi zako, mgeukie Bwana, akupe Roho Mtakatifu, akupe heshimu hiyo ya utakatifu. Hivyo Ikiwa upo tayari kufanya hivyo basi fungua hapa kwa ajili ya mwongozo wa sala ya toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA Bwana akubariki. Tafadhali shea na wengine ujumbe huu; Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
