NURU YA UPENDO
NURU YA UPENDO
February 11, 2025 at 04:29 PM
*MAOMBI YA USIKU.(JUMANANE.11.02.2025)* Shalom.Shalom. **NENO KUU* :UFALME WA MUNGU. Warumi:14:17 "Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu." Maombi Ya kila Siku Usiku Kuanzia saa Moja sio Ya kufunga unakula Chakula chako.ukitaka kulala./Kupumzika unaomba vipengele Vifuatavyo. *VIPENGELE VYA MAOMBI LEO JUMANNE.TUNAOMBA SALA YA BWANA KWA MFUMO MWINGINE .Luka 11:1-4, Mathayo 6 :9-13.* ✓ Mshukuru Mungu Kwa Siku Nzima Ya Leo Kwa uhai, Afya , Makanisa , Taifa , Familia, . ✓Omba Toba na Rehema . ✓Omba Utakaso Wa Roho ,Nafsi na Mwili . *1• UTUPE LEO. RIZIKI YETU.* Mathayo 6:11. Wagalatia 6:9-10 9 Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. 10 Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio. *✓Tusichoke* katika Kutenda Mema. ~•Omba Bwana afufue roho Zetu na Atujaze na upendo wake usioisha Kwa ulimwengu wenye uhitaji. *✓Tutavuna* Kwa Wakati Wake ,Tusipozimia roho . ~•Omba Mungu Alete Mavuno yake Katika Shamba lake .Luka 10:2. ~•Omba Bwana Aifanye Mikono Yetu kuwa na Uaminifu Tunapopanda na Kumwagilia Mbegu za Imani Kwa Wengine. *✓Tuwatendee* Watu wote Mema ~•Omba Mungu atupatie Macho ili Tuone fursa Kwa ajili Ya Huduma . ~•Omba Bwana atuoneshe Jinsi Ambavyo Tunaweza Kuonesha Upendo kwa Watoto wetu, Wenzi Wetu ,Marafiki zetu, Jirani Zetu na Kwa washiriki Wenzetu kanisani. ~ •Omba Mungu atupe Chakula Cha kutosha , Malazi ,Makazi, Afya , Kazi Na Fedha . *2•USITUTIE MAJARIBUNI.* Mathayo 6:13. Yakobo 1:13, "Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu." *✓Mungu* Hawezi Kujaribiwa Na Uovu. ~•Omba Mungu akupe nguvu ya Kuupinga na kuushinda Uovu . *✓ Wala yeye* Mwenyewe Hamjaribu Mtu. ~•Omba Mungu Usibaki katika Majaribu Ambayo Yanaweza Kukutenga mbali Naye. ~•Omba Mungu atufundishe kuzikimbia Tamaa za Ubinafsi zinazotushawishi na Kuelekeza Macho yetu kwenye tabia Yako isiyo na doa. ~•Omba Bwana Atuwezesha Kuchukia kile Anachokichukia na Kupenda kila anachokipenda. *3•UTUSAMEHE MAKOSA YETU.* Mathayo 6:14. *✓Mkiwasamehe* Watu Makosa Yao . ~•Wakati Fulani Hatutaki Kusamehe Kabisa .Omba Bwana Atuweke Huru kutoka Katika Uchungu na Chuki. ~•Omba Bwana Abadili Mioyo Yetu Na Airuhusu Neema Yake itiririke Kupitia Kwetu hadi Kwa wengine. ~•Omba Bwana Abadilishe Maadui Zetu Kuwa Marafiki Na Auunganishe Mioyo Yetu katika Huduma Kwa ajili Ya ufalme Wake . ✓ *Baba* Yenu Wa Mbinguni Atawasamehe Ninyi. ~•Omba Bwana Atufundishe Kupokea Msamehe Wake kwa Furaha na Kuieneza Neema hiyo Kwa Wengine . *N.b* . Funika nyumba Yako ,Kazi Yako, Elimu Yako ,uongozi wako ,ndugu zako, Watoto wako ,Kwa Damu ya Yesu .Na Vunja Kila maagano na uchawi na laaana Kwa Jina la Yesu . Mungu akitupa Neema kesho vipengele Vitatumwa . Mungu akubariki.
🙏 4

Comments