NURU YA UPENDO
February 12, 2025 at 03:32 PM
*MAOMBI YA USIKU*
( *JUMATANO.12.02.2025).*
Shalom.Shalom.
*NENO KUU:JIFUNZE KUOMBA.*
Luka 11:1
"Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake."
Mathayo 6:7-8.
Maombi Ya kila Siku Usiku Kuanzia saa Moja sio Ya kufunga unakula Chakula chako.ukitaka kulala./KUPUMZIKA unaomba vipengele hivi.
✓ Mshukuru Mungu Kwaajili Ya nguvu Wakati huu Wa Maombi .
✓Omba Toba na Rehema .
ZABURI 51:6.
✓Omba Utakaso Wa Roho ,Nafsi na Mwili .
1Wathesalonike 5:23.
*VIPENGELE VYA MAOMBI LEO JUMATANO.TUNAOMBA SALA YA BWANA MUENDELEZO.*
*1.JINA LAKO LITUKUZWE* .
Mathayo 5:16
"Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni."
*✓Nuru* Yenu Na Iangaze.
•Omba Bwana Atuwezeshe Kung'aa Kwa Mng'ao angavu Na Kwa Ujasiri ili wengine Wavutwe kwenye ufalme Wake Kupitia Upendo Wetu.
*✓Wapate* Kuyaona Matendo Yenu Mema.
•Omba Bwana Atuongezee upendo , Siyo Chuki Maishani Mwetu.
•Omba Bwana Atuoneshe Kuona Ukarimu Si Ubinafsi.
•Omba Mungu Kupitia Maisha Yetu ili Tuwabariki Watoto Wetu , Jirani Zetu , na Hata Adui Zetu.
*✓Wamtukuze* Baba Yenu Aliye Mbinguni .
•Omba Mungu Atufanye Sisi Tupungue, Yeye Aongezeke.
•Omba Bwana Atunyenyekeze na awasaidie Jiranizetu Kuona nguvu na huruma yako katika MatendoYetu ya upendo
*N.b* . Vunja na kuharibu roho za Wachawi, Ng'ome za Mapepo, Mauti , Vifo , Majanga , Magonjwa sugu na magonjwa ya kurithi ....Achilia Damu ya Yesu pande zote katika familia, kazi,elimu, biashara, Makanisa, Uongozi n.k.
Mungu akitupa Neema kesho vipengele vitatumwa .USIKU MWEMA.
Mungu akubariki.
🙏
❤️
9