
NURU YA UPENDO
February 17, 2025 at 04:01 PM
*MAOMBI YA USIKU*
( *JUMATATU 17•02.2025).*
Shalom.Shalom.
*NENO KUU* : *MKUMBUSHE BWANA KWA MAOMBI USIKAE KIMYA.*
Isaya 62:6-8
"Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha BWANA, msiwe na kimya;
7 Wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani.
8 BWANA ameapa kwa mkono wake wa kuume, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi."
✓ Mshukuru Mungu Kwa Makanisa, Familia, Taifa ,Afya , Nguvu ya Maombi kila siku Usiku anazokupa kuomba .
✓Omba Toba na Rehema .
ZABURI 51:1.
✓Omba Utakaso Wa Roho ,Nafsi na Mwili .
1 Wakorintho 7:1.
*VIPENGELE VYA MAOMBI LEO JUMATATU.👇👇*
*Fungua Anga la Mahali ulipo Kwa Jina La Yesu Na ita Damu ya Yesu Mahali hapo.*
*Fungua Siku Ya Jumatatu ya Leo mpaka JUMAPILI kila siku ifunike Kwa Damu ya Yesu.*
*1.Maombi ya Kujijenga Kiroho( Wafilipi 2:1-4).*
*✓Omba* Roho ya faraja Katika maisha Yako Katika Jina La Yesu.
*✓Omba* mapenzi ya Mungu juu ya maisha Yako yatimie Katika Jina La Yesu .
*✓Omba* ushirika wa Roho ukawepo ndani mwako Katika Jina La Yesu .
*✓Omba* Rehema kwa Bwana juu ya Maisha Yako Katika Jina La Yesu .
*✓Omba* furaha Katika Maisha Yako Katika Jina La Yesu .
*✓Omba* Nia Moja iwepo ndani mwako Katika Jina La Yesu .
*✓Omba* Mapenzi Mamoja Katika Mungu .
*✓Omba* roho Mmoja juu ya maisha Yako Katika Jina La Yesu .
*✓omba* unie Mamoja Katika yote Katika Jina La Yesu .
*✓ omba* Roho ya Unyenyekevu iwepo ndani ya roho Zetu Katika Jina La Yesu .
✓ *Omba* Mungu akupe moyo wa kumpenda jirani Yako kama Nafsi Yako..
*✓omba* Mungu akupe kuangalia mambo ya wengine walio na shida mfano wanaohitaji msaada wa kiroho , au wenye shida mbalimbali.
*✓ vunja* na kuharibu roho za Majivuno na mashindano Katika roho Zetu.
✓vunja na kuharibu Nguvu za Giza zinaondoa Roho ya faraja, mapenzi ya Mungu kwa waamini ndani ya roho zao, ushirika wa Roho, Nia Moja, mapenzi Mamoja, roho Mmoja n.k
✓. Vunja na kuharibu roho za Wachawi, Ng'ome za Mapepo, Mauti , Vifo , Majanga , Magonjwa sugu na magonjwa ya kurithi ....Achilia Damu ya Yesu pande zote katika familia, kazi,elimu, biashara, Makanisa, Uongozi n.k.
Mungu akubariki.
🙏
❤️
19