
NURU YA UPENDO
February 19, 2025 at 04:13 PM
*MAOMBI YA USIKU*
( *JUMATANO 19.02.2025).*
Shalom.Shalom.
*NENO KUU* : *KUTAFUTA AMANI* :
Waebrania 12:14.
"Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;"
✓ Mshukuru Mungu Kwa Makanisa, Familia, Taifa ,Afya , Nguvu ya Maombi kila siku Usiku anazokupa kuomba .
✓Omba Toba na Rehema .
✓Omba Utakaso Wa Roho ,Nafsi na Mwili .
*VIPENGELE VYA MAOMBI LEO JUMATANO* *KUHUSIANA NA KAZI ZINAZOTUINGIZIA KIPATO(Uchumi &Fedha ).👇👇* Muendelezo---.
■ *OMBA NGUVU YA ROHO MTAKATIFU NDANI YAKO ILI IKUSAIDIE KUMPASUA SIMBA ALIYE UTISHO KWAKO* ( Yaani hali mbaya ya kiuchumi iliyo UTISHO kwako ) na ILIYOSHIKILIA ASALI YAKO.
Kumbuka simba aliye uawa na Samsoni ndiye alikuwa amebeba ASALI. [ Asali =Uchumi, Fedha, Faida ]
●Roho ya Nguvu iliyomuijia Samsoni ndiyo iliyompa uwezo wa kumrarua simba na kula Asali akawapa na ndugu zake.
** *Omba ManenoHaya Kwa kumaanisha 👇*
✓Vunja kila roho iliyoshikilia Uchumi wako na biashara zako na Faida zako Kwa Jina la Yesu na Achilia Damu Ya Yesu .
■Navunja kila nguvu ya giza kwenye kazi zangu Kwa Jina la Yesu .
■Nakataa Kila roho ya Upofu kwenye kazi zangu Kwa Jina La Yesu
■Naipinga roho ya uvivu na ulegevu kwenye kazi zangu Kwa Jina La Yesu.
■Naharibu kila madhabahu ya Giza kazini kwangu Kwa Jina La Yesu .
■Roho ya Kupoteza naipinga kwa Jina la Yesu.
■Roho ya ugumu ninaiondoa kwa Jina la Yesu.
■Kila mawasiliano ya giza ofisi kwangu nayakata kwa Jina la Yesu.
■Natamka Neema na Baraka kazini kwangu Kwa Jina La Yesu .
" Roho ya BWANA ikamjilia kwa nguvu, naye akampasua kana kwamba anampasua mwana-mbuzi, wala hakuwa na kitu cho chote mkononi mwake; lakini hakuwaambia baba yake na mama yake aliyoyafanya." Waamuzi 14 :6
●Hiyo Roho ya Nguvu ndiyo ukupayo Utajiri na fedha.
"Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo." KUM 8:18
**Omba ManenoHaya Kwa kumaanisha 👇*
✓Mwambie Mungu akupe Nguvu za kusonga Mbele.
●Bwana Yesu naomba nijaze nguvu ndani yangu
●Naomba nguvu Katika, roho ,Mwili nafsi yangu
●Naomba nguvu Katika fikira, na mawazo yangu
●Naomba Nguvu Katika Nafasi Yangu
●Naomba nguvu zako
katikati ya maadui Zangu Isaya 62:7-8
●Naomba nguvu za Roho Mtakatifu Kwenye maamuzi yangu na matumizi yangu ya fedha.
●Mungu naomba nguvu zako kwenye kazi zangu
●Mungu nivike nguvu kwenye mikono yangu
●Kazi yangu ikawe na kibali kikuuu
●Neema ya nguvu KATIKA mambo magumu ikae ndani yangu
●Naomba nguvu ya fedha na utajiri.
●Aminaaa
■ *MWAMBIE MUNGU MANENO YAKO YAPATE KIBALI MBELE ZAKE.*
Maneno ya kinywa changu,Na mawazo ya moyo wangu,Yapate kibali mbele zako, Ee BWANA,Mwamba " Zaburi 19:14
Chochote ukichomueleza Mungu kwenye maombi haya na kikapate KIBALI mbele zake na Kukujibu. Amina.
■Mungu akubariki.
🙏
😂
4