Secar Sport
Secar Sport
February 3, 2025 at 11:42 AM
NAFASI YA KUCHUKUA UBINGWA BADO TUNAYO - MWAGALA Anaandika Afisa Habari wa Tabora United @mwagala.christina kupitia ukurasa wake wa Instagram “Bado nafasi ya kuchukua ubingwa tunayo”, akiamini kuwa timu hiyo inaweza kuwa bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu. Hii inakuja baada ya jana jioni kukubali kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya vinara wa Ligi hiyo Simba SC katika uwanja wao wa nyumbani Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora. Kwa sasa nyuki hao wa Tabora wanashika nafasi ya tano wakiwa na alama 25 baada ya kushuka dimbani mara 16 msimu huu, huku ratiba yao ikionyesha kuwa watashuka dimbani tena Jumatano ya wiki hii dhidi ya Namungo FC kutoka mkoani Lindi. Simba inakuwa timu pekee iliyopo katika top four ya Ligi msimu huu kuifunga Tabora United mpaka sasa baada ya Azam FC na Yanga SC wote kuangukia pua mbele ya Tabora huku Singida BS wakiambulia sare sare maua ya mabao 2-2.
Image from Secar Sport: NAFASI YA KUCHUKUA UBINGWA BADO TUNAYO - MWAGALA  Anaandika Afisa Haba...

Comments