
Secar Sport
22 subscribers
About Secar Sport
TAARIFA NA UCHAMBUZI KUHUSU MPIRA WA MIGUU NDANI NA NJE YA TANZANIA
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

Yanga sc kuendelea na safari yao ya kutetea ubingwa wa #NBCPremierLeague leo hii wakiwakaribisha Kagera sugar uwanja wa KMC complex (MWENGE) majira ya 10:00 jioni

Ligi kuu NBC premium league kurejea kesho kwa mchezo mmoja utakaopigwa Dar es salaam, klabu ya Yanga sc ikiwakaribisha wana supa nkurukumbi Kagera sugar. Mchezo utachezwa saa 10:00 jioni

Nyota wa Fountain Gate Selelmani Mwalimu amejiunga na klabu ya Wydad Casablanca kwa mkataba wa mwaka mmoja Sehemu ya makubaliaono ya mkataba huo Singida Black Stars atapata 10% ya mauzo ya mchezaji huyo kutoka kwa Wydad endapo mchezaji atauzwa Kwenda klabu nyingine ,kwani Selemani alikuwa katika klabu ya Fountain gates kwa mkopo akitokea Singida Black Stars. Mwalimu katika msimu huu wa 2024-2025 amefunga magoli 6 katika ligi kuu ya NBC akishika nafasi ya 3 katika orodha ya wafungaji bora

Taarifa zinaeleza kuwa ikiwa Yanga SC itawauza Stephane Aziz Ki na Clement Mzize basi watajaribu kumrejesha kikosini Zanzibar finest Feisal Salum Fei Toto. Lakini pia wataangalia namna ya kumsajili Djibril Sillah ambaye mpaka sasa hajasaini mkataba mpya na miamba ya Chamazi, Azam FC.

Droo kamili ya mechi za mchujo kutafuta timu 8 za kutinga hatua ya 16 bora Ligi ya Mabingwa barani Ulaya imepangwa, Manchester City itamenyana na mabingwa watetezi Real Madrid, huku Paris Saint-Germain wakichuana na wapinzani wa Ufaransa Brest. Mechi za kwanza za mchujo zimepangwa kufanyika Jumanne Februari 11 au Jumatano Februari 12. Mechi mkondo wa pili zitafanyika tarehe 18/19 Februari. Droo kamili ya hatua ya mchujo: 🛑Club Brugge vs Atalanta 🛑Sporting CP vs Borussia Dortmund 🛑🛑Man City vs Real Madrid 🛑Celtic vs Bayern Munich 🛑Juventus vs PSV 🛑Feyenoord vs Milan 🛑Brest vs PSG 🛑Monaco vs Benfica

🚨JE WAJUA...❓ Manchester United ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote mpaka sasa katika kampeni za kuwania kombe la UEFA Europa League ..

Kiungo shambuliaji wa kimataifa wa Zambia 🇿🇲 anayechezea klabu ya Yanga sc Clatous Chama amefichua kuwa pindi atakapokuwa anaelekea kustaafu soka ndoto zake ni kurudi kuichezea Simba kwa mara nyingine. “Nikikaribia kustaafu, timu ya kwanza kuipa kipaumbele cha kuichezea ni Simba ila kama wakinikataa ndio ninaweza kwenda timu nyingine kumalizia soka,”

Donald Ngoma (35) aliyewahi kuwa mchezaji wa Yanga sc pamoja na Azam Fc amejiunga na klabu ya Hardrock Fc ya Zimbabwe kwa mkataba wa mwaka mmoja akiwa kama mchezaji huru.