Secar Sport
Secar Sport
February 4, 2025 at 06:59 AM
🚨 Kocha mkuu wa klabu ya Heerenven Robin Van Persie ametoa malalamiko yake kwenda kwa shirikisho la mpira wa miguu nchini Uholanzi 🇳🇱 KVNB akidai kwenye Mchezo wa jumamosi klabu yake ilihujumiwa na waamuzi wote waliphusika kwenye mchezo dhidi ya Fortuna Sittard. Van Persie amedai kuwa dakika ya 88' ya Mchezo klabu ya Fortuna Sittard ilifanya mabadiliko ya wachezaji wawili lakini kwenye wale wawili waliotolewa Kuna mmoja hakutoka alibaki ndani ya pitch na kupelekea idadi ya wachezaji wa Fortuna Sittard kuwa 12 badala ya 11. Mpaka dakika ya 88' Heerenven walikuwa wanaongoza mabao 2-1 lakini dakika za 90c Fortuna Sittard walisawazisha na mechi kuisha 2-2. Picha mjongeo zinaoneshwa wachezaji wa Fortuna Sittard hawako sawa yaani wamezidi idadi inayotakiwa. Shirikisho la mpira wa miguu nchini Uholanzi litatoa taarifa rasmi kuhusu malalamiko ya Kocha Robin Van Persie ndani ya masaa 72 yajayo. ______________________________________
Image from Secar Sport: 🚨 Kocha mkuu wa klabu ya Heerenven Robin Van Persie ametoa malalamiko...

Comments