๐ข๐ง๐๐จ๐ ๐๐ก ๐๐๐๐ง
February 1, 2025 at 12:17 PM
Kwenye somo la Leo nimekutana na Challenge ya mmoja ya wafaitiliaji wangu, na Najibu Kwa niamba ya wote waliofikilia kama huyu.
Ni hivi, hoja yake ni zuri na yenye uzito. Kwa maana ya kwamba *Kuna watu wanapata pesa nyingi, wanazitumia vibaya, lakini bado pesa zinaendelea kuja kwao. Sasa swali ni. KWA NINI?*
Jawabu lake ni kwamba *MFUMO WAO WA MLANGO WA PESA NA MZUNGUKO WA NISHATI*
Pesa haziji kwa mtu kwa bahati tu. Hata wale wanaozitumia vibaya, mara nyingi wana mfumo fulani unaoendelea kuzalisha pesa kwao. Mfano:
- _Mfanyabiashara ana biashara inayoingiza faida kila siku, hata akizitumia zote, kesho zinakuja tena._
- _Mwanasiasa ana mirija ya mapato, akizitapanya leo, bado kuna nyingine zinaingia kesho._
- _Msanii au mtu maarufu ana mikataba na matangazo, akizimaliza leo, kesho anaingiza nyingine._
- _Mtu aliyerithi mali ana mfumo wa faida unaoendelea, hata akitumia vibaya, bado mapato yanaendelea kuja._
*Tofauti kati ya wenye pesa za kudumu na wale wanaozihangaika*
Tatizo linakuja kwa wale wasiokuwa na mfumo wa kuzalisha pesa, wale wanaoishi kwa kutegemea *BAHATI.* Wanaweza kupata pesa leo kwa njia ya mkopo, kamari, au mshahara wa muda, lakini kwa sababu hawana mfumo wa kuzizalisha upya, zikiondoka basi imekwisha.
Hoja hapa si kwamba pesa zinawapenda wale wanaozitapanya, bali ni kwamba *wameweka milango ya pesa wazi, hata kama wanazitumia vibaya, pesa bado zina njia ya kurudi.*
Je, wewe una mlango wa pesa unaoendelea kuingiza pesa hata zikiondoka? *Kama jibu ni hapana, basi ndio maana pesa hazikai au haziingii mara kwa mara.*
Swali la msingi sio _"kwa nini fulani anapata pesa hata akizitapanya?"_ Swali ni *"Mimi nimefungua mlango gani wa pesa kuja kwangu kwa utaratibu endelevu?"*
Ukiona mtu anakunywa kila siku lakini bado pesa zinaingia, usiangalie anavyotumia, angalia anavyozipata. *Mfumo wake ukoje?* Ukijifunza hilo, hautokuja kuhoji tena Bali ungeanza kutengeneza mfumo wako!
WhatsApp In-box ๐ https://wa.me/message/36OZ47M2H4RAA1
WhatsApp Channel OTHUMAN FACT Channel. ..https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s
๐
๐จ๐ฉ
๐ฎ
๐
5