𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧 WhatsApp Channel

𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧

610 subscribers

About 𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧

> Unahitaji maarifa ya maisha, mahusiano, heshima na mafanikio ya kweli? Jiunge na OTHUMAN FACT, channel inayogusa hisia, akili na maisha halisi. Kila siku tunakuletea uhalisia, ukweli na ushauri unaoweza kukusaidia kubadilika na kusonga mbele. BONYEZA HAPA KUJIUNGA. ..https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s *-Mimi naitwa OTHUMAN FACT, ni mshauri wa maswala yote ya kijamii Mahusiano/Mapenzi, Ndoa, Saikolojia, Biashara, Afya. Pia utapata kuelewa namna sahihi ya kuyaishi Maisha yako n.k Ahsante.* _Sevu namba ya WhatsApp Tuma Majina yako Ili kupata masomo ya ziada STATUS Bonyeza Link_ ..https://wa.me/message/36OZ47M2H4RAA1 Tuma Majina yako In-box. *Instagram* https://instagram.com/othumanfact?igshid=ZGUzMzM3NWJiOQ== *Facebook* https://www.facebook.com/profile.php?id=100075802703307&mibextid=ZbWKwL *TikTok* https://www.tiktok.com/@othuman.fact?_r= *WhatsApp Channel* https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s

Similar Channels

Swipe to see more

Posts

𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧
𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧
6/21/2025, 6:52:40 PM

Mafanikio yako ya kesho yanategemea zaidi uwezo wako wa kutoshikamana na mafanikio yako ya leo. Ameandika Othuman Fact Swala gumu sio ntapata nini ila nipo tayari kuacha nini ili nipate hicho ninachotamani. Issa alikuwa na utukufu wakiUngu lakini ili apate utukufu mkubwa zaidi alilazimika kutoshikama na utukufu aliokuwa nao akawa mwanadamu kisha alipomaliza akakirimiwa utukufu na enzi kubwa zaidi. Ulipo umeridhika ndio tatizo. Hutaki kuachilia ulichokishika ndio maana husogei. Tatizo sio shetani wala watu ila ni wewe uliyeendelea kubaki hapo ulipo. Usitumie nguvu nyingi kupambana KUWA bali tumia nguvu nyingi kupambana na vitu vinavyokuzuia KUWA. Hatupambani kuwa WATAKATIFU bali tunapambana na dhambi inayotuzuia kuwa watakatifu.. JIFUNZE... Usipambane kuwa mkuu bali ondoka kwenye mazingira yanayokuzuia kuwa mkuu. Usipambane kuwa mfanyabiashara mkubwa, ondoa tabia zinazokuzuia kufanikiwa kwenye ndoto yako hiyo. Usipambane kuwa mke/mume mwema, pambana na tabia zinazokufanya usiwe bora kwa mwenzi wako. Usipambane kuwa mtumishi, Sheikh, muhumini, mkubwa, we ondoa tu vile vikwazo vinavyokuzuia KUWA. Usipambane kuwa bora, ondoa tu vile vinavyokukwamisha kuwa mtu bora. Siri ni hii hapa; ACHA KUSHIKAMANA NA VITU/WATU/TABIA/FIKRA/HADHI zinazokukwamisha. Fanikiwa, shinda, kuwa mwema, kuwa mzuri na mwenye kuvutia, pata hekima, maarifa na ufahamu, kuwa na marafiki, kwazika, umizwa, jeruhiwa, juta, jilaumu, lala, ajiriwa, fanya biashara; ila inapokuwa swala la maisha yako jifunze KUTOSHIKAMANA na chochote kati ya hicho. Ikibidi kubadilika, badilika, ikibidi kuacha, acha na ikibidi kuondoka, ondoka. Follow na share kwa wengine πŸ‘‰ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s) β™‘ γ…€ Β  Β  βŽ™ Β  ⌲      πŸ”• *Κ³α΅‰α΅ƒαΆœα΅—Β Β Β  ˒ᡃᡛᡉ Β Β Β  ˒ʰᡃʳᡉ    α΅˜βΏα΅α΅˜α΅—α΅‰ αΆœΚ°α΅ƒβΏβΏα΅‰Λ‘*

𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧
𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧
6/21/2025, 2:55:22 PM
Post image
Image
𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧
𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧
6/21/2025, 6:20:48 AM

Hakuna wakati utakaokuwa *Sahihi kabisa kwako kuanza* kamwe hakuna siku utakuwa tayari kwa kila jambo unalotamani. Ukisubiri uwe tayari, utazeeka na ndoto zako. *Mambo makubwa yanaanza na hatua ndogo zilizoimara si mambo ya kusubiri uwe na hisia nzuri za kufanya hilo jambo.* Anza sasa hivi na kile ulicho nacho, Jenga nidhamu yako hata usipopewa motisha, Jifunze kujilazimisha hata kama hutaki, Nidhamu inakupa matokeo ambayo motisha haiwezi kukupa. Fanya kila siku kitu kinachokusogeza karibu na wewe wa kesho unayetaka kuwa. Usisubiri mpaka usifiwe, utazamwe. Jifunze kujiamsha mwenyewe, kujiongoza mwenyewe, kujituma mwenyewe. *Watu wakiona matokeo yako, ndio watakuamini. Lakini kabla ya hapo, ni lazima ujifundishe kuamini mwenyewe.* Kubadilika haimanishi unajaribu bahati, ni wewe kubeba majukumu. Weka mpango, jiweka wewe na malengo yako, ishi kwa kusudi. Hatima haiji kwa maombi, inakuja kwa mabadiliko ya tabia na maamuzi magumu unayokubali kuyasimamia kila siku. Kama utaanza leo, kesho haitakuwa kama jana. Na kila siku unayoshinda ukijijenga, inakusogeza karibu na mtu unayestahili kuwa. Follow na share kwa wengine πŸ‘‰ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s) β™‘ γ…€ Β  Β  βŽ™ Β  ⌲      πŸ”• *Κ³α΅‰α΅ƒαΆœα΅—Β Β Β  ˒ᡃᡛᡉ Β Β Β  ˒ʰᡃʳᡉ    α΅˜βΏα΅α΅˜α΅—α΅‰ αΆœΚ°α΅ƒβΏβΏα΅‰Λ‘*

πŸ‘ 1
𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧
𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧
6/20/2025, 2:00:32 PM

Follow na share kwa wengine πŸ‘‰ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s) β™‘ γ…€ Β  Β  βŽ™ Β  ⌲      πŸ”• *Κ³α΅‰α΅ƒαΆœα΅—Β Β Β  ˒ᡃᡛᡉ Β Β Β  ˒ʰᡃʳᡉ    α΅˜βΏα΅α΅˜α΅—α΅‰ αΆœΚ°α΅ƒβΏβΏα΅‰Λ‘*

Post image
πŸ’ͺ πŸ™ 2
Image
𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧
𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧
6/20/2025, 9:49:09 AM

Huwezi kupona kama hujaamua kukubali Ukweli, na kitendo Cha wewe kukubali Ukweli huo ndio mwanzo wa kupona kwako, ndio njia ya kuuanza mchakato wa kujiponya, huwezi kupona kama Bado unaendelea kujipa matumaini. Leo unaamua kuanza kumsahau mtu unajiwekea utaratibu wa Kuwa Unafuta namba kuwa hutomtafuta Tena Bado namba unaiandika pembeni ndo Unaifuta kwenye simu, alafu umejikaza baada ya wiki hivi unasikia kama moto unawaka ndani yako unatamani umetumia message hata hasipojibu unajipa matumaini umejiponya kwa kiasi, umekosea tayari unatakiwa kuanza upya, Sasa uwezi kupona kwa namna hiyo Ilo zoezi utalifanya hata miaka kumi ukitaka na Bado hautopona maumivu yako, Kumbuka hapa unaponya moyo maumivu yake hayasimuliki, ndo maana unaweza Kusema watu hawaelewi unavyojisikia, sio kwamba hawaelewi wanaelewa, uwezi kuukwepa mchakato huu wa maumivu Ili uhuponye moyo, unapoamua kufanya maamuzi Fanya husigeuke nyuma hiyo tanulu la moto linalowaka ndani yako unalilihisi wakati wa kujiponya ndo kupona kwenyewe husigeuke nyuma endelea mbeleπŸ’ͺ Follow na share kwa wengine πŸ‘‰ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s) β™‘ γ…€ Β  Β  βŽ™ Β  ⌲      πŸ”• *Κ³α΅‰α΅ƒαΆœα΅—Β Β Β  ˒ᡃᡛᡉ Β Β Β  ˒ʰᡃʳᡉ    α΅˜βΏα΅α΅˜α΅—α΅‰ αΆœΚ°α΅ƒβΏβΏα΅‰Λ‘*

πŸ‘ πŸ’ͺ πŸ™ 4
𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧
𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧
6/13/2025, 11:42:24 AM

πŸ’” MADA: Kwa Nini Mahusiano ya Siku Hizi Hayadumu? Tunapenda Vibaya au Tunapenda Watu Wasio Sahihi? *Vijana wengi leo wanaingia kwenye mahusiano lakini baada ya muda mfupi, mapenzi yanayeyuka shwaaaaaaah kama barafu.* *Wengine utawasikia wanasema tunapenda haraka, wengine wanasema tunapenda kwa macho.* *Lakini je, tatizo ni namna tunavyopenda au wale tunaowapenda?* Join *OTHUMAN FANS* https://chat.whatsapp.com/D0ekN0VYTz0I0a5egHpdqv

Post image
Image
𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧
𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧
6/13/2025, 2:39:15 PM

Kuna hii story ya Binti alimpenda kijana mmoja kwa moyo wake wote. Alikuwa tayari kujitoa, kumjali, na hata kumpa kidogo alichokuwa nacho ili kijana huyo asikose kitu. Huyu binti hakuwahi kumdai sana kijana huyo pesa wala vitu vya thamani kwake, mapenzi tu yalitosha. Lakini kadri muda ulivyopita, kijana alianza kubadilika. Simu hazipokelewi, ujumbe haujibiwi, na kila mara alikuwa na visingizio. Mwisho wa yote, kijana alimwambia huyu binti kwamba *Sijisikii tena kama awali, nataka muda.* Baada ya wiki mbili, huyu binti aliona picha za kijana huyo na msichana mwingine kwenye mitandao ya kijamii walikuwa kwenye hoteli ya kifahari, wakiwa wanakula BataπŸ˜‚, wakicheka kwa furaha. Kilichomuumiza zaidi Binti huyu. Ni kwa sababu alijitoa kwa mtu aliyekuwa na mipango tofauti na yeye. Sasa hii imenifanya niwaletee mada hii muijadili kutokana na hii story ya huyu binti *Kwanini mahusiano mengi siku hizi hayaendi mbali?* *Tunafanya kosa gani kama kizazi kuhusu mapenzi na mahusiano?* KARIBU SANA KATIKA *MADA* Hii MADA inaendeshwa katika group letu la *OTHUMAN FANS* Kama hujajiunga Bonyeza Link kwenye Post iliyopita kujiunga.

Post image
❀️ πŸ™ 2
Image
𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧
𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧
6/13/2025, 5:57:47 AM

*Usiyahukumu maisha yako kwa kuitumia mizani ya mtu mwingine. Kila mtu ana njia yake, Ana wakati wake, Ana mwelekeo wake, Kile ambacho wengine wamekipata leo, si lazima na wewe ukipate leo. Na kile ambacho hujakipata leo, si kwamba hutakipata kabisa.* Tatizo la kizazi chetu ni kuangalia pembeni wakati wa kuangalia mbele. Kila mtu anajua wapi mwingine kafika, lakini hajui anapotakiwa kufika yeye mwenyewe. Unajikuta una presha ya maisha ambayo hukuyachagua, unaingia katika mashindano ambayo hukuyasajili, unavaa kinyogo ambacho si chako. *Maisha ni ya mtu mmoja mmoja. Mshahara wa mtu mwingine haukupunguzii kipaji chako. Ndoa ya mtu mwingine haifuti utulivu wako wa sasa. Mafanikio ya rafiki yako hayakatai nafasi yako. Mungu hakosei ratiba kila kitu kinakuja kwa wakati wake.* Kujilinganisha kunaiua furaha yako, Kunatengeneza mashaka yasiyokuwa na sababu, Kunapofusha macho usione baraka zako, Huwezi kuishi kwa amani kama kila siku unajipima kwa viwango vya mitandao, watu, au matarajio yasiyo yako. *Jipende kwa hali uliyonayo sasa, Fanyia kazi maisha yako kimya kimya, Kuwa bora kwa mtazamo wako mwenyewe. Baraka zako haziko kwenye kulazimisha, ziko kwenye kuelewa na kuvumilia wakati. Hata jua halijawahi kushindani na mwezi, vyote vinang’aa kwa muda wake.* Follow na share kwa wengine πŸ‘‰ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s) β™‘ γ…€ Β  Β  βŽ™ Β  ⌲      πŸ”• *Κ³α΅‰α΅ƒαΆœα΅—Β Β Β  ˒ᡃᡛᡉ Β Β Β  ˒ʰᡃʳᡉ    α΅˜βΏα΅α΅˜α΅—α΅‰ αΆœΚ°α΅ƒβΏβΏα΅‰Λ‘*

Post image
πŸ™ 1
Image
𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧
𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧
6/13/2025, 7:07:44 PM

Follow na share kwa wengine πŸ‘‰ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s) β™‘ γ…€ Β  Β  βŽ™ Β  ⌲      πŸ”• *Κ³α΅‰α΅ƒαΆœα΅—Β Β Β  ˒ᡃᡛᡉ Β Β Β  ˒ʰᡃʳᡉ    α΅˜βΏα΅α΅˜α΅—α΅‰ αΆœΚ°α΅ƒβΏβΏα΅‰Λ‘*

Post image
Image
𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧
𝗒𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗑 𝗙𝗔𝗖𝗧
6/12/2025, 12:46:26 PM

Kabla hujaingia kwenye mahusiano, jiulize, *Ninajua Nini kuhusu mimi mwenyewe?* Namaanisha kuwa *huwezi kumjua unayemhitaji kama hujijui wewe mwenyewe ulivyo.* Ukijitafuta kwa mtu mwingine, utajipoteza ndani yake maana utakuwa unasimamia kivuli chake. Mapenzi ni ya watu wawili waliotoka sehemu tofauti, lakini wanaojua wanakoelekea ni wapi. Wengi wao wanaingia kwenye uhusiano wakiwa na hamu ya kupendwa, lakini hawajuhi wanataka nini. Ndiyo maana wanakubali chochote, wanavumilia kila kitu, na mwisho wa siku wanaishia kupigwa matukio na kulia peke yao, alafu wanaanza kujiuliza *Walikosea wapi?* Lakini kosa halikuwa kumpenda mtu, lilikuwa kutokujua thamani yako ni nini kabla ya kumpenda. Ukijijua kwanza inakusaidia kuchagua kilichobora, Unajua mipaka yako, Unajua kile usichotaka, Unajua tofauti kati ya kuvumilia na kuumizwa. Unajua upo kwenye mahusiano si kwa sababu ya kujitafuta, upo kwa sababu umekamilika na sasa uko tayari kushirikiana na mwenzi wako Katika kuzitimiza ndoto zenu. Kama leo ukijua wewe ni nani, hautalazimisha mapenzi. Huwezi kuwa na mahusiano yaliyo bora kama uliyaanzasha kwa sababu ni mpweke, unatapaswa kunanzisha mahusiano kwa sababu una utayari huo. Watu wawili wanaojijua, waliopona Majeraha yao na wakajifunza, ndiyo wanaoweza kujenga kitu cha kudumu. Ukitafuta mtu wa kukufanya ujisikie vizuri kabla hujajijua, utakuwa mfungwa wa hisia za watu milele. Jijue, Jipende, Jithamini. Ukitoka hapo, ukipenda utapenda kwa kuthamini, na hautakuwa na hofu ya kuachwa. Na utamvutia mtu anayeijua thamani yako kwa sababu tayari unaijua mwenyewe. Follow na share kwa wengine πŸ‘‰ [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s) β™‘ γ…€ Β  Β  βŽ™ Β  ⌲      πŸ”• *Κ³α΅‰α΅ƒαΆœα΅—Β Β Β  ˒ᡃᡛᡉ Β Β Β  ˒ʰᡃʳᡉ    α΅˜βΏα΅α΅˜α΅—α΅‰ αΆœΚ°α΅ƒβΏβΏα΅‰Λ‘*

Post image
❀️ 2
Image
Link copied to clipboard!