๐—ข๐—ง๐—›๐—จ๐— ๐—”๐—ก ๐—™๐—”๐—–๐—ง
๐—ข๐—ง๐—›๐—จ๐— ๐—”๐—ก ๐—™๐—”๐—–๐—ง
February 7, 2025 at 12:39 PM
*NINI KINATUFANYA TUWE BINADAMU?* Jua lilikuwa linazama huku upepo mwanana ukivuma taratibu. *Nilikuwa nimekaa kwenye benchi la bustani moja hivi la Manisipaa ya Geita, nikitafakari maisha.* Ghafla, nilimuona mzee mmoja mwenye ndevu nyeupe, akiwa amevaa shati jeupe lilikuwa limechakaa kidogo haikuwa ishu. Alikuwa amekaa pembeni yangu, akitazama watoto waliokuwa wakicheza mbali kidogo kutokea pale tulipokiwa sisi. Baada ya muda, niligeuka na kumsalimia. *โ€œShikamoo Mzee.โ€* Akajibu kwa sauti ya utulivu, *โ€œMarahaba kijana. Unaonekana una mawazo kidogo.โ€* Nikacheka kidogo na kusema, _โ€œNi kweli, mzee wangu. Nafikiria baadhi ya vitu kuhusu maisha.โ€_ Akatingisha kichwa kisha akasema, *โ€œUnajua, kijana wangu, maisha ni fumbo. Lakini kuna swali moja ambalo kila mtu anapaswa kujiuliza.โ€* Nikamuuliza, โ€œSwali gani hilo, mzee wangu?โ€ Akasema, *โ€œNINI KINATUFANYA TUWE BINADAMU?โ€* Nilikaa kimya kwa sekunde chache, nikijaribu kutafakari jibu. Nikaamua kusema, โ€œPengine ni akili zetu, uwezo wa kufikiria na kubuni baadhi ya mambo mapya.โ€ Mzee akatikisa kichwa kumaanisha, *โ€œHapana, wanyama pia wana akili zao. Ndege hujenga viota vya kushangaza, nyuki huunda mizinga kwa hesabu sahihi, na hata simba hujua kupanga mbinu za kuwinda.โ€* Nikajaribu tena, _โ€œPengine ni lugha, zetu maana sisi tunawasiliana kwa maneno na maandishi?โ€_ Mzee akatabasamu na kusema, *โ€œHata wanyama wana lugha zao. Mbwa hubweka kutuonya, nyani wanawasiliana kwa ishara, na nyangumi huwasiliana kwa sauti zao za kipekee."* Nikaanza kushindwa kupata jibu sahihi lipi, kisha nikamuuliza _, โ€œKwa hiyo, nini kinatufanya tuwe binadamu?โ€_ Mzee akavuta pumzi ndefu, kisha akasema, *โ€œNi uwezo wa KUJALI.โ€* Nikamtazama kwa mshangao, _โ€œUnamaanisha nini?โ€_ Akasema kwa upole, *โ€œBinadamu pekee ndiye anayejali hata asipokuwa na sababu ya moja kwa moja. Tunajali hata kuhusu watu tusiofahamu. Tunalia tukiona mateso ya wengine. Tunajitolea kusaidia pasipo kulazimishwa. Tunapenda, tunasamehe, na tunahangaika na mustakabali wa kizazi kijacho. Huu ndio Utu wetu.โ€* Nilikaa kimya nikitafakari maneno yake. Akaniangalia na kusema, _โ€œKijana, usiwe na haraka ya maisha. Usisahau kujali, kupenda, na kusaidia wengine. Hapo ndipo utakapogundua maana halisi ya kuwa binadamu.โ€_ Alisimama, akapiga hatua chache, kisha akageuka na kuniambia, *โ€œUsisahau, kijana. Ubinadamu siyo kazi, ni wito.โ€* Alipotokomea, nilihisi kama vile nimepokea somo kubwa maishani mwangu Kwa kwenda tu maeneo yale. *Kinachotufanya kuwa binadamu siyo akili, siyo lugha, siyo teknolojia, bali ni uwezo wetu wa kujali wengine hata kama hatunufaiki nao moja kwa moja.* WhatsApp In-box ๐Ÿ‘‡ https://wa.me/message/36OZ47M2H4RAA1 WhatsApp Channel OTHUMAN FACT Channel. ..https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s
Image from ๐—ข๐—ง๐—›๐—จ๐— ๐—”๐—ก ๐—™๐—”๐—–๐—ง: *NINI KINATUFANYA TUWE BINADAMU?*  Jua lilikuwa linazama huku upepo mw...
๐Ÿ™ โค๏ธ ๐Ÿ‘ ๐Ÿ’ช ๐Ÿค 9

Comments